Mbogwe kuibua kukabiliana changamoto ya ajira

Habari Leo
Published: Apr 24, 2025 09:24:26 EAT   |  Jobs and Career

HALMASHAURI ya wWilaya Mbogwe mkoani Geita, imezindua mashindano ya kusaka vipaji katika sekta ya sanaa na michezo kwa…

The post Mbogwe kuibua kukabiliana changamoto ya ajira appeared first on HabariLeo.

HALMASHAURI ya wWilaya Mbogwe mkoani Geita, imezindua mashindano ya kusaka vipaji katika sekta ya sanaa na michezo kwa vijana lengo likiwa ni kuwawezesha vijana kujiajiri na kukabilina na tatizo la ajira.

Mashindano hayo yanafahamika kwa jina la Fagason Festival 2025 yanafadhiliwa na wadau mbalimbali wa Maendeleo wilayani Mbogwe wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mashindano, Fagason Masasi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Fagason Festival 2025 iliyofanyika April 23, 2024 katika kata ya Nyakafuru, Fagason amesema mashindano hayo yanafanyika kwa awamu ya nne sasa dhamira ikiwa ni kukuza na kuendeleza vipaji.

Fagason amesema mashindano hayo yatagusa kata 17 za wilaya ya Mbogwe yenye vijiji 87 na vitongoji 386 ambapo washiriki na washindani wote watadahiliwa na jopo la majaji wabobezi ili kupata washindi sahihi.

Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbogwe, Pius Lukaga

Meneja wa Fagason Festival 2025, George Balele amesema zaidi ya washiriki 300 kutoka makundi mbalimbali wamethibitisha ushiriki wao katika mashindao hayo yenye dhamira ya kuwapa nafasi vijana kuonyesha vipaji vyao.

Mjumbe wa Kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbogwe, Pius Lukaga amepongeza hatua hiyo na kueleza mashindano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Wale tunaosoma vizuri Ilani ya Chama Cha Mpainduzi, Ibara ya 243 (i) inasema kwamba kubuni na kutekeleza mikakati ya kuwawezesha vijana waweze kushiriki shughuli za Maendeleo”, amesisitiza.

Akizindua mashindano hayo, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Ofisa Tarafa ya Masumbwe, William Lyanga amekiri kuwa mashindano hayo ni fursa nyingine kwa wahitimu wa chuo wasio na ajira.

Ofisa Tarafa ya Masumbwe, William Lyanga

Amesema kutokana na ongezeko la wasomi wengi kutoka ngazi ya shule za sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu, kuna uhaba wa ajira kwa wahitimu lakini wanaweza kujiajiri kupitia ubunifu na vipaji vyao.

“Kuna walemavu wanacheza michezo mbalimbali, kwa hiyo niwaombe kupitia mashindano haya, tuwatazame na hili kundi, ambao ni kundi maalum, tuwaibue na tuwaendeleze”, amesisitiza Lyanga.

The post Mbogwe kuibua kukabiliana changamoto ya ajira appeared first on HabariLeo.