Mbio za Kilimanjaro kuiweka Tz kwenye ramani

Habari Leo
Published: Oct 19, 2024 07:06:31 EAT   |  Travel

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amesema Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni chachu katika kukuza utalii na kuiweka Tanzania katika ramani ya riadha na utalii Kimataifa. Chana ametoa kauli hiyo usiku wa Oktoba 18,2024 wakati wa hafla ya kuzindua mbio za 23 za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon …

The post Mbio za Kilimanjaro kuiweka Tz kwenye ramani first appeared on HabariLeo.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amesema Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni chachu katika kukuza utalii na kuiweka Tanzania katika ramani ya riadha na utalii Kimataifa.

Chana ametoa kauli hiyo usiku wa Oktoba 18,2024 wakati wa hafla ya kuzindua mbio za 23 za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025 jijini Dar es Salaam.

“Mbio hizi za Kimataifa zenye washiriki zaidi ya 12,000 na wasindikizaji wao kutoka nchi zaidi ya 56 zimekuwa na manufaa makubwa kwetu, hasa katika kukuza utalii kwa kupitia michezo yaani sports tourism na kukuza uchum,” amesisitiza Chana.

SOMA: Kilimanjaro, Pwani zashinda dhahabu riadha UMISSETA

Amesema mbio hizo zimekuwa kichocheo cha kukuza uchumi kwani washiriki hutumia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwemo malazi, mawasiliano, usafiri, chakula, vinywaji na kadhalika hivyo kukuza uchumi wa wananchi wanaotoa huduma hizo.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na waandaaji wa Kilimanjaro Marathon ili kuona namna bora ya kutumia mbio hizo kuutangaza utalii zaidi na kuweka mikakati endelevu.

“Napendekeza tuangalie namna ya kufanya matangazo ya utalii kabla na baada ya mbio ili kuwaeleza watalii maeneo ambayo wanaweza kuzuru na kufurahia nchi yetu ili mapato yaongezeke kupitia utalii. Hii ni fursa adhimu ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii kwa watalii wa ndani na nje ya nchi,”Chana amesema.

Amesema mashindano hayo ya mbio ambayo  kufanyika chini ya Mlima Kilimanjaro ni tangazo tosha la kuwavutia watalii kuja nchini

Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania ,Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania, wadhamini wakiongozwa na mdhamini Mkuu Kilimanjaro Premium Lager, waandaaji wa mbio, wadau wa utalii na wawakilishi wa Jogging clubs.

The post Mbio za Kilimanjaro kuiweka Tz kwenye ramani first appeared on HabariLeo.