Mashindano ya Quran kutoa bodaboda, bajaji 

Habari Leo
Published: Feb 21, 2025 14:50:14 EAT   |  Sports

DAR ES SALAAM: MASHINDANO ya kusoma na kuhifadhi Quran yanayotarajia kufanyika Jumapili wiki hii yatawanufaisha washiriki 2000, huku…

The post Mashindano ya Quran kutoa bodaboda, bajaji  appeared first on HabariLeo.

DAR ES SALAAM: MASHINDANO ya kusoma na kuhifadhi Quran yanayotarajia kufanyika Jumapili wiki hii yatawanufaisha washiriki 2000, huku bodaboda, bajaji na magari watakaowahi Uwanjani watapewa kuponi maalumu kwa ajili ya kushindania zawadi hiyo.

Akizungumzia mashindano hayo Dar es Salaam leo, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema waandaaji wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhisha Quran nchini Tanzania chini ya Sheikh Othman Kaporo, yatagawa zawadi hizo kwa washiriki 2000 wa kwanza ambao watawahi na kupewa kuponi maalum kwa ajili ya kushindania zawadi hizo.

“Nimpongeze Shehe Kaporo kwa kuleta zawadi hizi ambazo kwa wale watakaobahatika zitawasaidia kwenye shughuli za kuzalisha Uchumi na kujikomboa kimaisha,” amesema.

SOMA ZAIDI: Rais Samia atoa Sh Mil 10 washindi mashindano ya Quran

Kamwe amesema mbali na hizo washiriki pia, watapewa zawadi za simu na washiriki wanne watapata safari ya kwenda Oman na Hijja.

Msemaji wa mashindano hayo Khamis Tembo amesema mgeni maalum Imamu kutoka Misikiti mitukufu ya Makkah na Madina aitwae Abdullah Ai Bu’ayjaan tayari amewasili nchini na leo alikuwa akisalisha katika Msikiti wa Mohamed wa VI.

Msemaji wa masuala ya dini wa Saudi Arabia Abdallah Al Enezi  amewahamasisha waislamu kuja kwa wingi kushuhudia tukio hilo la Jumapili linalofadhiliwa na wao.

Amesema mashindano hayo yanaonesha ukaribu mkubwa na ushirikiano mzuri baina ya nchi ya Saudia na Tanzania katika nyanja mbalimbali na moja muhimu ni sekta ya dini na masuala ya kutengeneza jamii na mafunzo ya Mwenyezi Mungu.

“Ufadhili wetu so tu wa kifedha tumeleta majaji watakaoshirikiana na Watanzania  na Baraza la Kiislam Tanzania katika masuala mbalimbali kuwanufaisha waislam,”amesema.

Mashindano hayo yataambatana na ugawaji wa tuzo za kitaifa na kimataifa ambako Vijana wenye umri wa chini ya miaka 12 kutoka mabara mbalimbali duniani wataonesha umahiri wao katika usomaji wa Quran.

The post Mashindano ya Quran kutoa bodaboda, bajaji  appeared first on HabariLeo.