Mashabiki ndio wanaumia! Kilio Arsenal wakipepetwa na kutupwa nje Uefa

LONDON, Uingereza
KILIO cha mashabiki wa Arsenal kuhusu kutoshinda taji kilifika miaka mitano sasa baada ya timu yao kupoteza nafasi kadhaa nzuri ikibanduliwa kwenye nusu-fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, Jumatano.
Wanabunduki wa Arsenal walisalimu amri ya Paris Saint-Germain kwa jumla ya mabao 3-1. Vijana wa kocha Mikel Arteta, ambaye anaaminika kukabiliwa na presha kwa sababu ya kutoshinda mataji, walipoteza 1-0 katika mkondo wa kwanza ugani Emirates kutokana na bao la Ousmane Dembele hapo Aprili 29.
Juhudi za kubadilisha matokeo katika mkondo wa marudiano ziliambulia patupu baada ya kuzamishwa 2-1 na miamba hao wa Ufaransa kupitia mabao ya Fabian Ruiz na Achraf Hakimi.
Timu zote mbili zilipoteza nafasi nzuri ikiwemo Vitinha kushuhudia penalti yake ikipanguliwa na kipa wa Arsenal, David Raya.
Hata hivyo, shujaa wa mipepetano ya nusu-fainali kati ya Arsenal na Inter alikuwa kipa Gianluigi Donnarumma aliyeondosha makombora kadhaa hatari ikiwemo katika mechi ya marudiano kutoka kwa Gabriel Martinelli, nahodha Martin Odegaard na Bukayo Saka aliyepata la kufuta machozi.
“Leo niliona kuwa wachezaji wangu walitaka sana ushindi kwa sababu walilia baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa. Nilizungumza nao na kuona uchungu waliohisi. Najivunia kazi yao kufika hapa. Sidhani kama kuna mtu alitarajia, lakini huu ndio umbali tulikaribia kufika utepeni,” akasema Arteta kabla ya kuongeza kuwa pia alisikitika na kukasirika kuwa hawakuweza kukamilisha kazi.
Arsenal sasa wamepoteza kwenye nusu-fainali mara nne mfululizo kwenye mashindano makubwa. Walipigwa breki katika hatua hiyo kwenye Ligi ya Uropa (2020-2021), League Cup (2021-2022 na 2024-2025) na Klabu Bingwa Ulaya (2024-2025).
Hakuna timu imecheza mechi nyingi kwenye Klabu Bingwa Ulaya bila kushinda taji kama Arsenal. Kwa kubanduliwa na PSG, Arsenal sasa hawana taji katika mashindano hayo ya haiba baada ya kusakata michuano 201.
Hata hivyo, Arsenal hawana muda wa kuomboleza kubanduliwa kwani nafasi yao ya kufuzu kwa mashindano hayo ya kimataifa msimu ujao bado si salama.
Wataingia ugani Anfield kuvaana na Liverpool hapo Jumapili wakiuguza kupigwa mara tatu mfululizo katika mashindano yote na pia kutoshinda michuano minne sasa.
Vijana wa Arteta wanapatikana katika nafasi ya pili ligini kwa alama 67 baada ya mechi 35 kusakatwa. Wanafuatiwa kwa karibu na Manchester City (64), Newcastle (63), Chelsea (63), Nottingham Forest (61) na Aston Villa (60).