Mariam Mwinyi azindua Zanzibar Afya Week

ZANZIBAR: MKE wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi amesema taifa linahitaji watu wenye afya bora ili kuwa mustakabali mzuri wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Mama Mariam ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF) amesema hayo alipoizindua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zanzibar …
ZANZIBAR: MKE wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi amesema taifa linahitaji watu wenye afya bora ili kuwa mustakabali mzuri wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mama Mariam ambaye pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Zanzibar Maisha Bora Foundation(ZMBF) amesema hayo alipoizindua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Zanzibar Afya Week’ Mkoa wa Mjini Magharibi Mei 8 2025.
Amesema kampeni hiyo ni fursa muhimu ya kuhakikisha wananchi wànapata huduma bora za afya ikiwemo elimu ya afya na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali Ikiwemo kisukari, presha, saratani ya matiti, macho na
oyo.
Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar Maisha Bora Foundation imejizatiti kushirikiana na Serikali kuimarisha huduma za afya na kuifanya Zanzibar kuwa na watu wenye afya bora na kituo muhimu cha utabibu kinachotambulika.
Aidha, Mariam Mwinyi amesema hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Afya hivi sasa zinaakisi dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi ya kuifanya Zanzibar kutoa huduma za matibabu, kupunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kufuata matibabu na kupunguza bajeti za matibabu na wageni wanaofika Zanzibar kupata huduma za uhakika za matibabu.
Halikadhalika Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa kupitia Kampeni ya Afya Bora Maisha bora ZMBF imeweza kuwafikia wananchi 21, 500 kupitia kambi nne za afya kuwapatia wananchi elimu ya afya, Unguja na Pemba.
Vilevile Zanzibar Maisha Bora Foundation imefanikiwa kupitia Mpango wa Lishe imeweza kuwafikia Wanawake 2,830 Unguja na Pemba kuwapatia elimu ya lishe, afya ya uzazi na mama wajawazito huduma za kliniki.
Kwa upande mwingine Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa Programu ya Tumaini Initiative ya ZMBF imeweza kuwafikia wasichana waliobalehe 8,676 Unguja na Pemba wa shule za msingi na sekondari na kuwapatia tumaini kits na elimu ya hedhi salama.
Mama Mariam Mwinyi amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika kuimarisha hospitali na vituo vya afya pamoja na sera na teknolojia ya utoaji wa huduma katika sekta ya afya na kuipongeza kwa mafanikio hayo.
Uzinduzi huo uliambatana na Programu za Lishe Bora 2025, Afya Mama na Mtoto 2025 na Sheria Afya Programu 2025.