MAONI: Upinzani unavyoweza kuepuka kuvurugwa na Ruto kabla ya uchaguzi wa 2027

KATIKA siasa za Kenya, kugawanyika kwa upinzani si jambo geni, hasa ikizingatiwa uwezo wa rais aliye madarakani kutumia mbinu mbalimbali kupunguza ushindani uchaguzini.
Rais William Ruto, ambaye ameonyesha ustadi mkubwa wa kisiasa, anaendelea kujijenga kuvuruga umoja wa upinzani kuelekea uchaguzi wa 2027 kwa kupanda fuko wake ndani ya upinzani.
Ili kukabiliana kikamilifu na mbinu hizi za Ruto, viongozi wa upinzani wanahitaji mikakati ya kisiasa iliyo thabiti, kudumisha umoja, na kuwa na malengo ya dhati ya pamoja.
Umoja ni silaha kuu ya upinzani dhidi ya serikali yoyote iliyo madarakani.
Viongozi wa upinzani wanapaswa kuweka tofauti zao za kibinafsi na za vyama kando ili kuunda muungano wa kweli unaojengwa juu ya maono ya pamoja kwa taifa.
Wanahitaji kujifunza kutokana na historia, ambapo upinzani umepoteza mwelekeo kwa sababu ya kushindwa kuweka maslahi ya taifa mbele ya matakwa ya kibinafsi au ya vyama.
Viongozi wa upinzani wanapaswa kuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na kujenga utaratibu wa ushirikiano ulio wazi na thabiti.
Serikali mara nyingi hutumia ahadi za nyadhifa, rasilimali, au miradi ya maendeleo kama mbinu za kuvuruga muungano wa upinzani.
Ili kuepuka mitego hiyo, upinzani unapaswa kuweka misingi imara ya maadili kwa wanachama wake.
Pia, vyama vya upinzani vinafaa kuwa na mkataba wa kisiasa wa wazi kudumisha maadili kuzuia wanachama kuhamia upande wa serikali.
Upinzani unapaswa kuimarisha mawasiliano na wananchi kupitia vuguvugu la kisiasa lililo hai, kwa njia ya mikutano, mitandao ya kijamii, na majukwaa ya kiraia.
Kukumbatia ajenda zinazowagusa wananchi, kama vile gharama ya maisha, ukosefu wa ajira, na ufisadi.
Mojawapo ya mbinu kuu ambazo serikali hutumia ni kutokuwepo kwa mgombea wa pamoja wa upinzani.
Kufikia 2026, vyama vya upinzani vinapaswa kuwa tayari vimeanza mchakato wa kumsaka na kumwidhinisha mgombea wa urais wa pamoja ili kuepuka migawanyiko ya dakika za mwisho.
Kwa kushirikiana na mashirika ya kijamii na jamii ya kimataifa, upinzani unaweza kupata ulinzi wa kidiplomasia dhidi ya mashambulizi ya kisiasa na udhalimu wa serikali.
Asasi hizi pia zinaweza kusaidia kudumisha utawala wa sheria na kutoa shinikizo kwa serikali kuheshimu demokrasia.
Kuepuka kuvurugwa na kugawanywa na Rais Ruto kunahitaji uongozi wa upinzani uwe makini, wenye maono, na ujasiri wa kisiasa.
Ni kupitia mshikamano wa kweli, maadili ya kisiasa, na uhusiano wa karibu na wananchi ndipo upinzani utaweza kujenga nguvu za haja kumenyana na Ruto 2027.
Wakati ni sasa wa kujifunza kutokana na makosa ya zamani, na kuunda upinzani wenye nguvu unaoweza kushindana vikali na serikali ya Kenya Kwanza.