Manispaa Geita yavuka 90% ukusanyaji mapato

GEITA: HALMASHAURI ya Manispaa ya Geita imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 18.05 sawa na asilimia 93.06 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 19 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Muyenzi amesema hayo Mei 14, 2025 katika kikao cha nne cha Baraza la Madiwani …
GEITA: HALMASHAURI ya Manispaa ya Geita imefanikiwa kukusanya kiasi cha Sh bilioni 18.05 sawa na asilimia 93.06 ya lengo la kukusanya Sh bilioni 19 za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Muyenzi amesema hayo Mei 14, 2025 katika kikao cha nne cha Baraza la Madiwani kwa mwaka huu wa fedha na kueleza takwimu hizo ni hadi Aprili 30, 2025.
Muyenzi amesema tayari kiasi cha Sh bilioni 7.2 ya mapato hayo ya ndani kimeshaelekezwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo miradi ya elimu, afya, kilimo, miundombinu na biashara.
Amesema mbali na mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha pia manispaa ya Geita imepokea kiasi cha sh bilioni 2.63 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii.
Ameeleza pia wamepokea kiasi cha sh milioni 204 kati ya Sh milioni 422 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) ya Pesa za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutekeleza miradi viporo ambayo haikukamilika kati ya mwaka 2018-2021.
Ameeleza pia wamepokea kiasi cha sh milioni 204 kati ya sh milioni 422 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) ya Pesa za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutekeleza miradi viporo ambayo haikukamilika kati ya mwaka 2018-2021.
Meya wa Manispaa ya Geita, Costantine Morandi amesema makadirio ya mapato ya ndani yamepanda kwa sh bilioni 11 ndani ya miaka mitano kutoka Sh bilioni 5 mwaka 2020 hadi sh bilioni 19 mwaka 2025.
Ameongeza pia ndani ya kipndi cha mwaka mmoja makadirio ya mapato yamepanda kwa sh bilioni tano, kutoka sh bilioni 14 kwa mwaka 2023/24 hadi kufikia Sh bilioni 19 kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Amesema hatua hiyo imepanua uwezo wa manispaa kutoa mikopo ya vikundi maalum kutoka kukopesha sh milioni 698 mwaka 2020 hadi kufikia uwezo wa kukopesha kiasi cha Sh bilioni 1.78 kwa mwaka 2025.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Michael Msuya akizungumza kwa niaba ya chama ameipongeza halmashauri na kukiri wazi kuwa viongozi waliopewa dhamana ndani ya manispaa wanawajibika.