Majuto Mlimani kwa kukosa chama cha kisiasa chenye nguvu

Taifa Leo
Published: Nov 03, 2024 03:55:37 EAT   |  News

KUONDOLEWA kwa Rigathi Gachagua kutoka wadhifa wa Naibu Rais kumezidisha kampeni ya kubuniwa kwa vyama vya kisiasa mahususi vya eneo la Mlima Kenya. Baadhi ya wanasiasa wanadai masaibu ya mbunge huyo wa zamani wa Mathira yalichangiwa na eneo hilo kuunga mkono chama cha United Democratic Alliance (UDA) moja kwa moja bila kupitia chama chao cha kisiasa. Kando na mgawanyiko katika ya Mlima Kenya Magharibi na Mlima Kenya Mashariki, chama hicho kinakabiliwa na kibarua cha kurejesha imani ya wakazi kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Kampeni ya eneo la Mlima Kenya kuwa na chama chake mahususi ilianza mapema mwaka huu baada ya kuripotiwa kuwa Bw Gachagua alikuwa ameanzisha mchakato wa kutwaa chama cha The New Democratics (TND) baada ya uhusiano kati yake na rais William Ruto kuanza kuzorota. Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, mwandani wa karibu wa Bw Gachagua, amesema anasikitika kuwa “hatukuungana na Rais Ruto kupitia chama cha kisiasa” mnamo 2022. “Kuna vyama vingi zaidi vya asili ya Mlima Kenya. Ikiwa hali itakuwa ngumu, tunaweza kujiunga na moja ya vyama tulivyogura Jubilee na kujiunga na UDA,” Bw Kahiga akasema mnamo Agosti 2024. Gavana wa zamani wa Kiambu Ferdinand Waititu pia amekuwa akihimiza kuwa wakazi wa Mlima Kenya wajiunge na chama kimoja cha asili ya eneo hilo. Alitoa pendekezo hilo Julai mwaka huu kufuatia hatua ya Rais Ruto kuteua viongozi wa chama cha ODM kuwa mawaziri katika serikali yake. “Sharti eneo la Mlima Kenya lidhamini mgombea urais kwa tiketi ya chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Ikiwa kutakuwa na mazungumzo, yafanyike tukiwa ndani ya chama chetu. Hatuwezi kurudia kosa tulilotenda 2022 kwa kujiunga na UDA bila makubaliano,” Bw Waititu akasema. Hivi maajuzi, Bw Gachagua alisema Rais Ruto amemsaliti kwa kuruhusu abanduliwe mamlakani ilhali alimsaidia kushinda uchaguzi wa 2022. “Tulipokuwa tukiunda UDA, nilimwamini Rais Ruto lakini wanasiasa wengine walisisitiza kuwa na mkataba wa maelewano kati yao na yeye. Ninashangaa kwamba Rais Ruto niliyemsaidia kushinda uchaguzi anaweza kunitendea mabaya kiasi hiki,” Gachagua akasema. Waziri wa zamani wa Kilimo Mithika Linturi pia amesema ataunga mkono wazo la kubuniwa kwa chama mahususi kutetea masilahi yao. “Kama viongozi, sharti tutengeneze nyumba yetu na tujipange vizuri. Tusishawishiwe tujiunge na vyama vya watu. Mambo yakiharibika mwenyeji atakurusha nje na hautakuwa na la kufanya. Tusirejelee kosa hilo mnamo 2027,” Bw Linturi akasema. Kauli sawa na hilo imetolewa na kiongozi wa chama cha PNU Peter Munya aliyesema kuwa Gachagua alitimuliwa kwa urahisi kwa kukosa chama chake. “Kuondolewa mamlakani kwa Gachagua ni funzo kubwa kwetu. Ukiingia ndani ya nyumba ya mtu, anaweza kukurusha nje wakati wowote akitaka. Tusipotoshwe ila tuwe na makubaliano chini ya chama chetu. Hii ndio maana tumehifadhi PNU,” Bw Munya, ambaye ni Gavana wa zamani wa Meru, akasema. Kwa hivyo, Profesa Kindiki anaingia mamlakani kama mwanasiasa kutoka Mlima Kenya mwenye cheo cha juu zaidi serikalini, wakati ambapo viongozi wa eneo hilo wamepoteza imani na serikali anayoihudumia. Japo wabunge 69 mnamo Septemba walimtawaza Profesa Kindiki kuwa msemaji wa eneo la Mlima Kenya serikalini, anakabiliwa na changamoto ya kuzima hasira za wakazi na ushawishi wa Gachagua. Hii ni licha ya kwamba utendakazi wake ulisifiwa na wengi akihudumu kama Waziri wa Usalama. Imetafsiriwa na Charles Wasonga