Mabomba ya umwagiliaji shamba la Mbegu (ASA) Msimba yaungua moto

Milard Ayo
Published: Sep 19, 2024 15:01:38 EAT   |  Sports

Zao la mbaazi katika shamba la wakala wa Mbegu (ASA) Msimba lililopo Wilaya ya Kilosa Mkaoni Morogoro zimenusurika kutetekea kwa moto baada ya mtu asiyejulikana kuwasha moto shamba hilo na kuunguza miundombinu ya umwagiliaji mabomba zaidi ya 15. Akizungumza mbele ya mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka,meneja wa shamba hilo Samson Moleli amesema […]

The post Mabomba ya umwagiliaji shamba la Mbegu (ASA) Msimba yaungua moto first appeared on Millard Ayo.

Zao la mbaazi katika shamba la wakala wa Mbegu (ASA) Msimba lililopo Wilaya ya Kilosa Mkaoni Morogoro zimenusurika kutetekea kwa moto baada ya mtu asiyejulikana kuwasha moto shamba hilo na kuunguza miundombinu ya umwagiliaji mabomba zaidi ya 15.

Akizungumza mbele ya mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka,meneja wa shamba hilo Samson Moleli amesema moto huo umeanza tangu septemba 14 mwaka huu Kisha kuthibitiwa na Jana septemba 18 kuzuka Tena kwa mara nyingine.

Amesema licha ya moto huo kuharibu miundombinu ya umwagiliaji lakini pia umechoma sehemu ndogo ya shamba la Mbegu za mbaazi ambazo zipo kwenye majaribio ya awali kabla ya kupelekwa Kwa wananchi.

Moleli amesema kwa Sasa wamewekeza nguvu kwenye kuthibiti moto huo licha ya mara nyingi kuzuka majira ya usiku ambapo hadi Sasa chanzo chake hakijajulikana.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ameagiza vyombo vya usalama kuchunguza chanzo cha moto huo ambao umekua ukizuka Kila mwaka katika shamba hilo nyakati kama hizi za maandalizi ya msimu wa Kilimo.

DC Shaka amesema pamoja na kuendelea kutoa elimu Kwa wananchi kuacha tabia hiyo ya kuchoma moto hovyo lakini amewataka ASA kuimarisha Ulinzi katika mashamba hayo ambayo ndio tegemeo kubwa kwa Taifa katika uzalishaji mbegu za mazao mbalimbali.

The post Mabomba ya umwagiliaji shamba la Mbegu (ASA) Msimba yaungua moto first appeared on Millard Ayo.