Maafisa wa Gavana Wavinya Ndeti wakamatwa na EACC

MAAFISA wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), Alhamisi, Aprili 3, 2025 walivamia afisi kadhaa katika Kaunti ya Machakos, na kuondoka na stakabadhi.
Uvamizi huo, ulisababisha mvutano huku askari wa kaunti waliosaidiwa na polisi wawili wa utawala, wakiwatishia wanahabari waliokuwa wakifuatilia msako katika afisi za Waziri wa Fedha wa kaunti Bw Onesmus Kuyu, katika makao makuu ya Machakos.
Inadaiwa kuwa wapelelezi hao walimchukua Bw Kuyu kutoka nyumbani kwake jijini Nairobi.
Pia, walivamia afisi za Katibu wa Kaunti ya Machakos Bw Muya Ndambuli na afisi za Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Miji, Bw Nathaniel Nganga, kabla ya kuelekea katika Hospitali ya Rufaa ya Machakos.
Akithibitisha msako huo, mkuu wa mawasiliano wa EACC, Bw Stephen Karuga, alisema ni sehemu ya uchunguzi kuhusu madai ya ufisadi.
“Tume inachunguza madai kadhaa ya ufisadi yanayowahusu maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Kaunti ya Machakos. Operesheni hii ni sehemu ya mchakato wa uchunguzi unaoendelea ili kukusanya ushahidi muhimu wa kuthibitisha madai hayo. Watuhumiwa wataandikisha taarifa,” alisema Bw Karuga.
Hatua hii ya EACC inajiri chini ya wiki moja baada ya Bw Kuyu kukanusha madai ya ufisadi alipofika mbele ya kamati ya ukaguzi katika Bunge la Machakos.
Bw Kuyu alitii wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya wiki kadhaa za kujificha na kukwepa maswali ya Wawakilishi wa Wadi.
Wakati wa kikao hicho, Bw Kuyu alikuwa na wakati mgumu kujieleza.
Alisema maafisa wa serikali ya kaunti walio wafisadi na wasio jua majukumu yao wanapaswa kubeba mizigo yao wenyewe.
Madai ya ufisadi yanaendelea kusababisha mgawanyiko kati ya makundi mawili ya Wawakilishi wa Wadi.
Kundi moja limetishia kumng’oa Spika wa Bunge la Kaunti ya Machakos, Bi Anne Kiusya, likimtuhumu kwa kutokuwa na uwezo wa kuongoza na kusakata ufisadi.
Wakati huohuo, kundi jingine linamshutumu Gavana Ndeti, kwa kushindwa kuruhusu ufisadi kuenea.