Kituo cha kujaza gesi CNG chakamilika asilimia 90

Habari Leo
Published: Mar 03, 2025 11:39:45 EAT   |  News

BODI ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) imesema kituo mama cha kushindilia na…

The post Kituo cha kujaza gesi CNG chakamilika asilimia 90 appeared first on HabariLeo.

BODI ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) imesema kituo mama cha kushindilia na kujaza gesi asili (CNG) kimekamika kwa zaidi ya asilimia 90 na hivi karibuni kitaanza kutoa huduma.

Kauli hiyo ilitolewa leo Machi 3, 2025 jijini Dar es salaam na Mkurungenzi wa Mipango na uwekezaji TPDC, Derick Moshi kwa niaba ya Mkurungenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mussa Makame alipotembelea kituo hicho kujiridhisha kama kimekidhi vigezo vinavyohitajika kabla ya kuanza kutumika.

“Kituo kimekamilika na tuko hatua za mwishoni kabisa na kama mnavyojua hii ni gesi unapoingiza sehemu yeyote lazima ifatilie sana hatua za mwisho ili isitokee ikavuja sehemu yeyote kwa ajili ya usalama wa magari na watu waliopo kwahiyo ni zaidi ya asilimia 90 iliyofikiwa na tayari gesi ipo hapa….ni kwamba hatujaingiza gari kutokana na kutaka kujiridhisha zaidi,”amesema Moshi.

Ameongeza,”Kabla ya mwezi huu kukamilika tutakuwa tumemaliza kila kitu na tutazindua,”

Akimwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC,Balozi Ombeni Sefue,Paul Makanza amesema bodi imeridhishwa na maendeleo ya kituo mama hicho kwani kukamilika kwake kunaisaidia serikali kupunguza gharama za ununuzi wa mafuta kutoka nje ya nchi.

“Kwanza niipongeze Manejimenti kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha mradi huu unakamilika hivi karibuni kwani kutakuwa na workshop itakayokuwa inamilikiwa na Chuo Kikuu hivyo hii ni fursa nzuri,”amesema Makanza.

Ameongeza,”Mradi huu ni muhimu sana kwa sababu gesi asilia ni mbadala wa mafuta na kama mnavyojua serikali inapata mafuta kutoka nje na inatumia fedha za kigeni hivyo mradi huu utasaidia kupunguza gharama za kutoa mafuta hayo nje na kuokoa fedha hizo na mradi utakapokuwa mkubwa utasambaa nchi nzima na kukuza uchumi wa nchi,”

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio amesema mradi wa kituo hicho unaojengwa katika eneo la Ubungo mkoani Dar es salaam umegharimu jumla ya Sh bilioni 14.5

The post Kituo cha kujaza gesi CNG chakamilika asilimia 90 appeared first on HabariLeo.