Kitendawili cha kimya cha Nyoro huku Ruto na Gachagua wakiambiana kwaheri

Taifa Leo
Published: Nov 03, 2024 04:55:07 EAT   |  News

MUUNGANO wa Kenya Kwanza ulipoingia mamlakani mwaka wa 2022, mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro alianza kuonyesha azma kuu ya kisiasa. Wafuasi wake, hata hivyo walitamauka alipokosa kuteuliwa katika Baraza la Mawaziri la kwanza la Rais William Ruto baada ya uvumi kuibuka kuwa angekuwa miongoni mwa watu waliopendekezwa kwa wadhifa mkubwa. Hii, wengine walidhani, ingekuwa zawadi kwa mwanasiasa huyo aliyekuwa kwenye orodha ya mchujo ya mgombea mwenza wa Dkt Ruto pamoja na Prof Kithure Kindiki - wadhifa ambao hatimaye Rigathi Gachagua alitwaa. Hata hivyo, Bw Nyoro hatimaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati yenye nguvu ya Bajeti na Matumizi ya Bunge la Kitaifa. Rais katika mikutano yake mingi ya hadhara aliandamana na Bw Nyoro na katika hotuba zake, Dkt Ruto alimtambulisha kuwa “kijana mwenye nyota inayong’aa kisiasa.” Katika matamshi mengi hadharani, wafuasi wa Bw Nyoro wakati huo, wakiongozwa na Seneta wa Murang'a Joe Nyutu, walitaka Bw Gachagua atimuliwe na nafasi yake kuchukuliwa na mbunge huyo wa Kiharu mwenye umri wa miaka 38. Kisha yakaja maandamano ya kitaifa ya Gen Z mwezi Juni, yakichochewa na Mswada wa Fedha wa 2024 ambapo vijana walitaka rais ajiuzulu. Kamati ya Bw Nyoro ilikuwa na jukumu muhimu katika mpango huo wa ushuru uliozua utata, pamoja na Kamati ya Fedha inayoongozwa na Mbunge wa Molo, Kimani Kuria. Maandamano Kufikia wakati rais alipotupilia mbali Mswada wa Fedha wa 2024, na kuvunja baraza lake la mawaziri na kuanzisha msako dhidi ya wale aliowataja kuwa 'wahalifu wasaliti walioshiriki maandamano', Bw Nyoro alinyamaza. Kisha kukaja hoja dhidi ya Bw Gachagua ambapo Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse, akiungwa mkono na wabunge 291, aliwasilisha hoja ya kumtimua madarakani Bw Gachagua. Saini ya Bw Nyoro haikuwa miongoni mwa wabunge waliounga mkono hoja hiyo.Bunge la Seneti lilifuata muda mfupi baadaye kupiga kura ya kumuondoa Gachagua ofisini. Hata hivyo, katika kipindi chote cha dhoruba hiyo, Bw Nyoro amesalia kimya.Kutimuliwa kwa Bw Gachagua kulipoidhinishwa na Seneti na wakati wa Rais Ruto kumchagua mrithi wake ukawadia, baadhi walilitaja jina la Bw Nyoro miongoni mwa wawaniaji. Badala yake, ni Gavana wa Murang’a Irungu Kangata aliyeonekana kumenyania wadhifa huo.Rais alipomteua Prof Kindiki, Bi Maina alichapisha kwenye mitandao ya kijamii ujumbe akisema “tulimuuliza (Ndindi) Nyoro ikiwa bado ana nia ya kiti kikubwa lakini akasema hawezi kumkosea heshima Naibu Rais (Bw Gachagua)”. Aliongeza: 'Hatukuwa na chaguo jingine ila kumwacha. Tulimsihi Seneta Nyutu ajiunge nasi, lakini alikataa na kusema atakuwa pale Bw Nyoro anaegemea'. Bw Nyoro hakujibu mara moja maswali kutoka kwa Taifa Jumapili. Huku ukimya wa Bw Nyoro ukiendelea kuvutia hisia kwa madai kwamba alikuwa tikitimaji kisiasa asiye na msimamo wowote, kuna wanaoamini anafaa kueleza msimamo wake ili kuepuka utata. Imetafsiriwa na Benson Matheka