Kisa idadi ya wapiga kura RT, viongozi wakimbilia kwa Prof Kabudi

Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) imeweka wazi inashindwa kutangaza tarehe ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi Mkuu kwa sababu kuna baadhi ya viongozi hawakuridhika na maamuzi yaliyofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Katiba hivyo kuandika barua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Palamagamba Kabudi kupinga maamuzi ya mkutano huo.