Kilichoiua Simba Morocco hiki hapa, yapewa nondo za kuibeba nyumbani

MCHEZO wa fainali ya mkondo wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika baina ya RS Berkane dhidi ya Simba umemalizika nchini Morocco kwa wenyeji kushinda 2-0, hivyo kwa sasa ni kuuendea wa marudiano utakaochezwa Tanzania, Jumapili ijayo huku yakibainika mambo matatu yaliyoigharimu timu hiyo.