Kigoda cha JICA kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini

KIGODA cha Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kimezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo…
The post Kigoda cha JICA kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini appeared first on HabariLeo.
KIGODA cha Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kimezinduliwa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambacho ni jukwaa la wataalamu kubadilishana ujuzi na kufanya tafiti juu ya mbinu bora za kilimo cha umwagiliaji.
Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk Wilson Mahera, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dk Mahera amesema hatua hiyo itasaidia wataalamu kupata mbinu za kisasa, hasa kutokana na mafanikio ya Japan katika kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu – SUA (Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu), Prof. Maulid Mwatawala, amesema kuwa kigoda hicho kitaleta mchango mkubwa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini.
Naye Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mikami Yoichi, amesema kuwa kigoda hicho kitaimarisha uelewa wa uzoefu wa maendeleo ya Japan na mchango wake kwa Tanzania kupitia mihadhara, semina na tafiti mbalimbali.
Mwakilishi Mkazi wa JICA, Asano Seizaburo, ameongeza kuwa kigoda hicho ni fursa muhimu ya kubadilishana utaalamu na kusaidia kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji nchini Tanzania.
The post Kigoda cha JICA kuimarisha kilimo cha umwagiliaji nchini appeared first on HabariLeo.