Kibali chatafutwa kutwaa mali inayohusishwa na ‘Mathe wa Ngara’

MALI ya mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati Nancy Indoveria Kigunzu, almaarufu 'Mathe wa Ngara' sasa itatwaliwa ikiwa ombi lililowasilishwa mahakamani litakubiliwa.
Katika ombi lake katika Mahakama Kuu, Shirika la Kutwaa Mali ya Wizi (ARA) linataka liruhusiwe kutwaa magari matatu ya kifahari, jumba la makazi lililoko Juja na zaidi ya vipande tisa vya ardhi vinavyoaminiwa kuwa mshukiwa huyo aliinunua kwa pesa alizopata kutokana na uhalifu.
ARA inasema kuwa 'Mathe wa Ngara' alihamisha na kusajili baadhi ya mali hiyo kwa majina ya washirika wake na jamaa zake wa karibu kwa lengo la kuhujumu uchunguzi unaoendelea.
“Uchunguzi umebaini kuwa kuna sababu ya kuamini kuwa mali hizo zilipatikana kupitia biashara haramu ya dawa za kulevya na hivyo zilitokana na uhalifu,” shirika hilo likaeleza katika ombi lake.
Mnamo Novemba mwaka jana, ARA ilifaulu kupata agizo la mahakama lililomzuia Bi Kigunzu na washirika wake kuuza, kuhamisha umiliki au kuendesha shughuli zozote katika mali hizo.
Kipande cha ardhi kilichoko eneo la Juja-Kalimoni, Kaunti ya Kiambu kinamilikiwa na Bi Kigunzu na kusajiliwa kwa jina la George Jumba Inguti na ploti nyingine katika eneo hilo lilisajiliwa kwa majina ya Bw Inguti na Scolastica Wambui Kibathi.
Shirika la ARA linataka kutwaa na kuirejeshea serikali vipande vingine vitatu vya ardhi vilivyoko Chavakali, kaunti ya Vihiga.
Kupitia wakili wake Benard Gitonga, ARA inasema kuwa Bi Kigunzu alisajili mali hizo kwa majina ya washirika wake, ili kuficha asili ya pesa zilitumika kuzinunua.
Shirika hilo lilisema lilianzisha uchunguzi dhidi ya mshukiwa huyo baada ya kukamatwa kwake mnamo 2023 na kushtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya.
Baadaye polisi walivamia jumba hilo la Juja na kupata dawa hizo na vifaa vingine katika chumba kilichoitwa “control room”. Maafisa hao waliwakamata washukiwa zaidi ambao wameshtakiwa kwa ulanguzi wa mihadarati.
ARA ilisema mienendo ya Bi Kigunzu ya kubadili umiliki ya mali hizo na kuzisajili kwa majina ya washirika wake, ilikuwa ithibati ya juhudi zake za kuficha manufaa aliyopata kutokana na biashara hiyo haramu.
Mwaka jana Bi Kigunzu alipoteza Sh13.4 milioni zilizotwaliwa kutoka nyumbani kwake, baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa zilipatikana kutokana na biashara haramu.
Tafsiri: CHARLES WASONGA