Kamati yakagua miradi ya bil 2.5/- Nanyamba

Habari Leo
Published: Jan 07, 2025 13:20:50 EAT   |  News

MTWARA: KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa…

The post Kamati yakagua miradi ya bil 2.5/- Nanyamba appeared first on HabariLeo.

MTWARA: KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani humo yenye thamani ya Sh bilioni 2.5.

Akizungumza leo katika halmashauri wakati kamati hiyo ya siasa mkoani humo ilipotembelea miradi hiyo ya maendeleo, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara, Mobutu Malima amesema lengo la kukagua miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Miradi iliyotembelewa kwenye halmashauri hiyo ikiwemo ya elimu, maji pamoja na afya ambayo tayari imeshakamilika na wananchi wanaendelea kupata huduma.

Aidha akiwa katika mradi wa zahanati ya kijiji cha Milangominne kwenye halmashauri, katibu huyo amewapongeza wananchi hao kwa kuanzisha wazo na kuona umuhimu wa kujenga zahanati hiyo lakini pia nguvu zao walizotumia kwa ajili ya ujenzi huo.

Licha ya jitihada na pongezi hizo zilizotolewa kwenye mradi huo wa zahanati lakini bado ujenzi unakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo miundombinu ya umeme, maji, vifaa tiba na vingine hivyo katibu huyo ameuagiza mkurugenzi wa halmashauri kuwa baada ya miezi mitatu wakirudi wakute mabadiliko makubwa katika ujenzi huo.

“Naomba nitoe rai baada ya miezi mitatu tukute maji, umeme na tukute marekebisho yote niliyoyaona mule ndani yawe yamekamilika angalau tutoe matumaini kwa wananchi wanapokuja kutibiwa hapa,”amesema Mobutu.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwemo Somoe Mbwana ameipongeza serikali kwa kuendelea kujali afya za wananchi hao na kuwaletea mradi huo ambao sasa unaenda kuwapunguzia adha ya kwenda vijiji jirani kufata huduma ya afya ikiwemo kijiji cha mnyawi na vingine.

The post Kamati yakagua miradi ya bil 2.5/- Nanyamba appeared first on HabariLeo.