Kabudi azindua bodi ya ithibati ya waandishi wa habari

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameizindua rasmi Bodi ya Ithibati…
The post Kabudi azindua bodi ya ithibati ya waandishi wa habari appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameizindua rasmi Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, ambayo imekuwa ikisubiriwa tangu mwaka 2016.
Bodi hiyo italenga kusaidia waandishi wa habari kushughulikia changamoto na migogoro yao ya kitaaluma kabla ya kufikishwa mahakamani.
Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 03, 2025 jijini Dar es Salaam, ukiwahusisha wawakilishi mbalimbali kutoka sekta ya habari nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Kabudi amesisitiza kuwa bodi hii ni hatua muhimu katika kuimarisha weledi wa taaluma ya uandishi wa habari, kuchochea uwajibikaji, kulinda haki za waandishi wa habari na kuhakikisha waandishi wanapata fursa ya kusuluhisha matatizo yao kwa njia ya kitaalamu na ya haki.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau wa habari, waandishi wa habari, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zinazohusika na sekta ya habari nchini.
The post Kabudi azindua bodi ya ithibati ya waandishi wa habari appeared first on HabariLeo.