Jux Azindua EP Yake “A Day To Remember”

DAR-ES-SALAAM : MSANII nyota wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu kama Jux, ameendelea kuandika historia ya mapenzi kwa kuzindua EP yake mpya “A Day To Remember”, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha ndoa yake na mpenzi wake Priscy.
DAR-ES-SALAAM : MSANII nyota wa Bongo Fleva, Juma Mkambala maarufu kama Jux, ameendelea kuandika historia ya mapenzi kwa kuzindua EP yake mpya “A Day To Remember”, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha ndoa yake na mpenzi wake Priscy.
Uzinduzi wa EP hiyo umetanguliwa na mfululizo wa sherehe sita za kifahari zilizofanyika nchini Nigeria, huku kilele cha harusi kinatarajia kufanyika Mei 28, 2025, katika ukumbi wa Super Dome, Masaki – Dar es Salaam.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux amesema kazi hiyo ni zaidi ya burudani ya muziki kwani inasimulia safari ya upendo wao, urithi wa kitamaduni na furaha wanayoshiriki kama wanandoa.
EP hiyo inajumuisha nyimbo zilizoandaliwa kwa kushirikiana na wasanii mahiri barani Afrika, akiwemo Phyno kutoka Nigeria na D Voice kutoka Tanzania, ikiwa ni juhudi za kuunganisha sauti na ladha za Afrika Mashariki na Magharibi.
Watayarishaji walioshiriki kuunda EP hiyo ni pamoja na S2kizzy, Foxx Made It, na Aykbeats, huku Lizer Classic akisuka mixing na mastering kwa ubora wa hali ya juu.
SOMA: Jux asogeza mbele uzindua wa albamu
Katika salamu zake za shukrani, Jux alimpongeza mke wake, familia, timu nzima ya usimamizi na mashabiki kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha kazi hiyo. Aliahidi pia kutoa wimbo maalum kama zawadi kwa mashabiki wake mara baada ya kufunga ndoa rasmi jijini Dar es Salaam.