JKCI kutumia mashine ya ECHO kuziba moyo
DAR-ES-SALAAM : WATAALAMU wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamepewa mafunzo jinsi ya kuziba matundu na…
The post JKCI kutumia mashine ya ECHO kuziba moyo appeared first on HabariLeo.
DAR-ES-SALAAM : WATAALAMU wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wamepewa mafunzo jinsi ya kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba bila ya kufanya upasuaji wa kufungua kifua na kutumia mashine zenye mionzi.
Upasuaji huo unafanyika kwa njia ya tundu dogo kwa kutumia mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO).
Akizungumza kuhusu mafunzo hayo yaliyotolewa jijini Dar es Salaam, Prof. Xiangbin Pan ambaye ni Mkurugenzi Mkuu kutoka hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China, Prof. Pan amesema wagonjwa wengi wa moyo wako vijijini na wanazifuata huduma za matibabu na upasuaji mijini mahali ambako kuna hospitali kubwa zenye wataalamu wabobezi, kufanyika kwa upasuaji huo kunawapunguzia wananchi gharama ya kusafiri na kukaa hospitali muda mrefu.
“Kuwepo kwa teknolojia hii kumetusaidia kuwatibu kwa urahisi wagonjwa wa moyo kwani tunatoa huduma hii katika hospitali na tunawafuata wagonjwa mahali walipo na kuwafanyia upasuaji ndani ya gari maalumu ambalo ndani yake kuna chumba cha upasuaji pamoja na mashine za ECHO kwaajili ya kufanya upasuaji huo”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge ameshukuru kwa mafunzo yaliyotolewa na kusema kuwa kuwepo kwa utaalamu huo kutaokoa maisha ya wagonjwa wengi zaidi na kupunguza gharama za matibabu.
Dkt. Kisenge amesema ushirikiano uliopo kati ya China na Tanzania ni wa muda mrefu na unafaida nyingi moja ya faida iliyopo ni katika sekta ya afya ambapo serikali ya China ilijenga jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kila baada ya miaka miwili madaktari bingwa kutoka nchini humo wanakuja hapa nchini kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi.
“Matibabu haya ni ya teknolojia ya hali ya juu na ni rahisi kufanyika kwani hayatumii mionzi ambayo inaweza kusababisha madhara kwa mgonjwa pamoja na mtoa huduma na yanapunguza gharama za matibabu”.
Daktari bingwa wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Ludovick ambaye alipata mafunzo hayo kwa muda wa miezi mitatu katika ya Hospitali ya Fuwai nchini China amesema utaalamu alioupata ni wa hali ya juu na atautumia kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
“Nimejifunza jinsi ya kutumia mashine ya ECHO kuziba matundu ya moyo ambayo ni teknolojia ya kisasa, inayomlinda mgonjwa na mtoa huduma kutokupata madhara yatokanayo na mionzi pia mgonjwa anapata huduma ya matibabu kwa gharama naafuu ukilinganisha na njia ya kutumia mionzi”, amesema Dkt. Theophylly.
Dkt. Theophylly amesema teknolojia hii ya upasuaji inafanyika kwa watu wazima na watoto wenye matatizo ya tundu kwenye moyo.
Mafunzo hayo yanakwenda sambamba na kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo kwa watoto, ambapo wataalamu wa JKCI na wenzao wa hospitali ya Fuwai watashirikiana kutoa huduma hiyo
The post JKCI kutumia mashine ya ECHO kuziba moyo appeared first on HabariLeo.