Israel yashambulia Taasisi za Hezbollah

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 14:31:05 EAT   |  Business

LEBANON : JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya anga yaliyolenga taasisi ya fedha inayodaiwa kuhusika kwa ufadhili wa silaha za wapiganaji wa Hezbollah wakati wakiendelea kutanua mashambulizi nchini Lebanon. Mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga  matawi ya taasisi ya Al-Qard Al-Hassan  katika miji ya Nabatiyeh na Tyre. Hatahivyo, taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel  imedai …

The post Israel yashambulia Taasisi za Hezbollah first appeared on HabariLeo.

LEBANON : JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya anga yaliyolenga taasisi ya fedha inayodaiwa kuhusika kwa ufadhili wa silaha za wapiganaji wa Hezbollah wakati wakiendelea kutanua mashambulizi nchini Lebanon.

Mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga  matawi ya taasisi ya Al-Qard Al-Hassan  katika miji ya Nabatiyeh na Tyre.

Hatahivyo, taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel  imedai kuwa maeneo kadhaa ya taasisi hiyo yakiwemo matawi yake ya benki yalikuwa yakitumiwa na wapiganaji wa Hezbollah.

Mashambulizi haya yanaashiria  kutanuka kwa vita vya Israel dhidi ya Hezbollah katika kupunguza uwezo wa kundi hilo kuendesha operesheni zake.

Taasisi hiyo inafahamika kwa kutoa mikopo nchini Lebanon ambako mifumo ya kawaida ya kibenki ilisambaratika miaka mitano iliyopita kutokana na mgogoro mbaya wa kiuchumi.

SOMA : Israel yashambulia ngome za Hezbollah

 

The post Israel yashambulia Taasisi za Hezbollah first appeared on HabariLeo.