Iran kusaini mkataba wa kimkakati na Urusi
URUSI : RAIS wa Iran, Masoud Pezeshkian, amewasili nchini Urusi kwa mazungumzo na Rais Vladimir Putin na pia…
The post Iran kusaini mkataba wa kimkakati na Urusi appeared first on HabariLeo.
URUSI : RAIS wa Iran, Masoud Pezeshkian, amewasili nchini Urusi kwa mazungumzo na Rais Vladimir Putin na pia kusaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Habari la Serikali ya Urusi, TASS, imesema mazungumzo yao yatagusia mahusiano ya mataifa hayo pamoja na masuala ya kimataifa kabla ya kusaini makubaliano hayo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Pezeshkian nchini Urusi tangu aliposhinda uchaguzi mwezi Julai mwaka uliopita, baada ya kifo cha mtangulizi wake, Ibrahim Raisi.
Urusi imekuwa ikitafuta ushirikiano na Iran pamoja na mataifa mengine yanayoshirikiana na Marekani kama Korea Kaskazini, tangu kuzuka kwa vita nchini Ukraine.
Urusi tayari imeingia makubaliano ya kimkakati na Pyongyang, mshirika wake wa karibu Belarus pamoja na China. SOMA: BRICS Pay kubadili mfumo wa kimataifa wa malipo
The post Iran kusaini mkataba wa kimkakati na Urusi appeared first on HabariLeo.