Huzuni mpenzi wa zamani akishambulia kipusa na kumuacha bila mikono  

Taifa Leo
Published: Dec 30, 2024 11:19:50 EAT   |  News

POLISI katika Kaunti ya Taita Taveta wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja kutoka eneo la Voi, alijeruhiwa na mpenziwe wa zamani baada ya mtafaruku kutokea kati yao. Bi Asha Orimbo, mwenye umri wa miaka 35 kutoka eneo la Voi, hana sababu ya kusherehekea sikukuu kwani alijipata hospitalini akipata matibabu ya majeraha makubwa. Akiongea na Taifa Dijitali katika kijiji cha Gaza, mjini Voi, alisema kuwa alikuwa na matumaini makubwa ya kusherehekea sikukuu na wapendwa wake, lakini mambo yaligeuka. Mwanzoni mwa mwezi huu wa Desemba, mpenziwe ambaye wamekuwa pamoja kwa takriban mwaka mmoja alikatiza uhusiano wao na kuamua kumwacha. Kulingana na Bi Asha, hakuona sababu yoyote ya yeye kutatiza uhusiano huo. Kutokana na hasira za kuwachwa, Desemba 12, aliamua kuvamia nyumba ya mpenzi wake saa tano usiku na kuanza kurusha mawe kwenye mlango wake. Jamaa huyo, akiwa na hasira kali, aliamka, akachukua panga na kumkimbiza na kumkata mikono yote miwili na kumwacha akivuja damu. “Nilipiga nduru sana na kwa bahati nzuri wapita njia walikuja, kisha wakamjulisha ndugu yangu ambaye alimwambia babangu. Nilipata majeraha makubwa kwani alinikata mikono yote,” alieleza. Babake alimkimbiza katika hospitali ya Moi mjini Voi ambapo alipata matibabu ya haraka. “Nilikuwa na hasira sana aliponiambia anataka kumaliza uhusiano wetu na kurudi kwa mkewe. Ananiwachaje wakati wa sikukuu?” alihoji huku akijaribu kulazimisha tabasamu. “Sijui kwa nini aliamua kuniacha bila sababu yoyote ya maana,” alitaka kujua, akitikisa kichwa. Alisema maumivu ya kimwili ni makali, lakini maumivu ya moyoni yalikuwa makubwa zaidi kwani aliyemshambulia alikuwa mtu aliyemjua na kumwamini, na kufanya usaliti huo kuwa wa uchungu zaidi. Alisema kuwa tayari ametoa taarifa kwa vyombo vya usalama katika kituo cha polisi cha Voi na kuwataka wachukue hatua za haraka. “Nataka akamatwe ili ajutie alichonifanyia. Babangu aliniambia kuwa polisi walisema lazima nipone kwanza kabla mshukiwa akamatwe na kushtakiwa,” alisema. Babake, Bw Athman Orimbo, alieleza uchungu wake kuhusu tukio hilo akisema familia sasa inaishi kwa hofu kuwa mshambuliaji, ambaye bado hajakamatwa, anaweza kujaribu kuwadhuru.  