Hongera Rais Samia, TFF kukamilisha maandalizi CHAN

Habari Leo
Published: Dec 21, 2024 07:47:58 EAT   |  Sports

KUPATA nafasi ya kuandaa fainali za Mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) au zile za mataifa…

The post Hongera Rais Samia, TFF kukamilisha maandalizi CHAN appeared first on HabariLeo.

KUPATA nafasi ya kuandaa fainali za Mabingwa wa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) au zile za mataifa ya Afrika (AFCON) ni jambo moja na kukamilisha maandalizi yake ni jambo lingine.

Tanzania tumekamilisha maandalizi ya michuano ya Chan inayotarajia kuanza Februari mwakani baada Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuthibitisho hilo juzi.

Rais wa Caf, Patrick Motsepe kwenye ukaguzi wake Uwanja wa Benjamin Mkapa juzi alisema anaondoka Tanzania
akiwa na furaha kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika.

Alimpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kuwekeza kwenye maandalizi.

Kama Motsepe anampongeza Rais Samia na Karia kwa kukamilisha maandalizi ya michuano ya Mabingwa Afrika sisi pia tunaungana nae katika kuwapongeza.

Kukamilisha kwa wakati maandalizi ya michuano hii kunatoa taswira ya kwamba hata ile ya Afcon, ambayo Tanzania
kwa kushirikiana na Uganda na Kenya wataandaa mwaka 2027 pia yako kwenye mikono salama.

DCIM100MEDIADJI_0038.JPG

Tunamtia moyo Rais Samia na Karia kuendelea pale walipoishia kwenye maandalizi ya Chan kuelekea Afcon,
ushirikiano wao na wa wadau wote umefanikisha mafanikio haya makubwa katika Taifa la Tanzania.

Na hii italeta imani si kwenye mchezo wa mpira wa miguu tu bali hata kwa michezo mingine kwamba Tanzania ni
sehemu sahihi ya kupewa dhamana ya kuandaa mashindano mbalimbali.

Wahenga wanasema hata mbuyu ulianza kama mchicha, ndivyo ambavyo nasi tunaitazama Tanzania kwa miaka
kadhaa ijayo.

Wamepewa dhamana ya kuandaa michuano hii mikubwa basi hatuna shaka siku moja watakuja kupewa dhamana ya
kuandaa mashindano mengine makubwa kwa siku za usoni kwa sababu tayari wameonesha kuwa wanaweza.

Aidha, ukamilifu huu wa maandalizi ya michuano ya Mabingwa wa Afrika tunaamini unaenda sambamba kabisa na kuandaa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ikiwezekana kuandika rekodi ya kushinda ubingwa huo kwenye ardhi ya nyumbani.

Si kitu rahisi kushinda ubingwa huo lakini pia tunaamini si jambo linaloshindikana kama dhamira na maandalizi ya
kitaalamu yatafanyika kwa Taifa Stars.

Hongereni Rais Samia na Karia kwani dhamira yenu, ushirikiano wenu wa bega kwa bega umefanikisha kukamilika
kwa maandalizi ya michuano hii.

The post Hongera Rais Samia, TFF kukamilisha maandalizi CHAN appeared first on HabariLeo.