Hatuondoi walinda amani – UN

Habari Leo
Published: Oct 15, 2024 16:54:34 EAT   |  General

NEW YORK : UMOJA wa Mataifa umegoma kuondoa walinda amani wake kusini mwa Lebanon na wataendelea kuwepo kusaidia raia wa Lebanon licha ya matakwa ya Israel  yakutaka  walinda amani hao kuondolewa katika eneo hilo. Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewaambia waandishi wa habari mjini New York kwamba …

The post Hatuondoi walinda amani – UN first appeared on HabariLeo.

NEW YORK : UMOJA wa Mataifa umegoma kuondoa walinda amani wake kusini mwa Lebanon na wataendelea kuwepo kusaidia raia wa Lebanon licha ya matakwa ya Israel  yakutaka  walinda amani hao kuondolewa katika eneo hilo.

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amewaambia waandishi wa habari mjini New York kwamba uamuzi wa kuacha kikosi vya UN kuendelea kuwepo katika nafasi yake umeungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi wanachama zinazochangia wanajeshi katika kikosi hicho.

Mwishoni mwa wiki hii , Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliutaka Umoja huo  kuondoa kambi zake kusini mwa Lebanon, ambazo alidai kuwa zinatumika kama ngao kwa wapiganaji wa Hezbollah.

Hatahivyo, Mkuu  wa ulinzi na amani wa Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix amesema  vikosi vya Umoja wa Mataifa  havitaondoka na vitaendelea kutekeleza majukumu yake kama walivyopewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kusaidia raia.

Hatahivyo, Israel imehoji kuwa Umoja wa Mataifa umeshindwa kuwazuia Hezbollah kujenga mahandaki na kuweka silaha kama maroketi na makombora karibu na mpaka na kwenda kinyume na makubaliano ya awali waliyokubaliana.

Umoja wa Mataifa umesema jukumu kubwa la Umoja wa Mataifa ni kusaidia pande zote mbili zenye mzozo na sio kutekeleza makubaliano.

SOMA: UN, Lebanon waomba ufadhili dola mil 426

Hatahivyo, Umoja wa Mataifa umeendelea kuishutumu Israel kwa kulenga vituo vyake kimakusudi, huku walinda amani watano wakijeruhiwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita, tuhuma ambazo Netanyahu amekanusha.

The post Hatuondoi walinda amani – UN first appeared on HabariLeo.