Gathungu ararua utekelezaji wa mipango ya Ruto

MKAGUZI Mkuu wa Hesabu za Serikali, Nancy Gathungu, ametoa tathmini kali kuhusu Ajenda ya Mageuzi ya Kiuchumi ya kuanzia mashinani (BETA) ya Rais William Ruto, akiitaja kama safari isiyoweza kufanikiwa.
Ripoti yake, iliyowasilishwa bungeni, inaibua wasiwasi kuhusu mafanikio ya mpango huo, ambao ulikuwa msingi wa kampeni za Rais Ruto kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.
"Ripoti za ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Kifedha wa 2023/2024 za idara za serikali zinazohusika na nguzo kuu za BETA, pamoja na mashirika ya serikali yanayosaidia nguzo hizo, zimeonyesha wasiwasi kuhusu utendaji wao, zikibainisha dosari na mapungufu yanayoweza kuathiri mafanikio ya mpango wa BETA ikiwa hayatatatuliwa," inasoma sehemu ya ripoti hiyo.
Mpango wa BETA unazingatia nguzo tano kuu: mageuzi ya kilimo; biashara ndogo, na za kati (MSMEs); afya; makazi na mpango wa ujenzi wa nyumba; pamoja na mpango mkuu wa kidijitali na sekta ya ubunifu.
Mpango huu umelenga kushughulikia changamoto zinazokumba uchumi wa nchi, kuchochea ukuaji wa kiuchumi, na kujenga uthabiti wa kiuchumi. Unalenga pia kupunguza gharama ya maisha, kuunda nafasi za ajira, kuhakikisha ugavi sawa wa mapato, kuboresha usalama wa kijamii, kupanua ukusanyaji ushuru na kuongeza mapato ya fedha za kigeni.
Mambo yanayowezesha utekelezaji wa nguzo hizi ni pamoja na uchumi wa majini, elimu na mafunzo, mazingira na mabadiliko ya tabianchi, sera za kigeni na ujumuishaji wa kikanda, utawala, miundombinu, viwanda, huduma, ajenda ya wanawake, ulinzi wa kijamii, michezo, utamaduni na sanaa, pamoja na uwezeshaji wa vijana.
Katika sekta ya kilimo, ambayo ni nguzo kuu ya mpango huu, Bi Gathungu ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu changamoto zinazokwamisha mafanikio yake.
Masuala yaliyojitokeza ni pamoja na usambazaji wa mbolea duni, mchakato wa ununuzi usio wa kawaida, ukosefu wa stakabadhi sahihi na visa ambapo mbolea ilinunuliwa lakini haifikishiwi kwa wanaolengwa.Mpango wa ruzuku ya mbolea ulianzishwa katika mwaka wa kifedha wa 2021/22 kama hatua ya kusaidia wakulima dhidi ya kupanda kwa bei ya pembejeo.
"Ripoti za ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Kifedha wa 2023/2024 kwa idara ya kilimo na mashirika husika ya serikali kama Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao zimegundua changamoto zinazoweza kudhoofisha utekelezaji wa nguzo hii," ripoti inasema.
"Pia, kuna wasiwasi kuhusu usahihi wa orodha ya wakulima walionufaika, ucheleweshaji wa kukamilika kwa miradi, na dosari katika mchakato wa ununuzi wa vifaa vya kukaushia nafaka na miundombinu yake. Changamoto hizi zinaweza kuhatarisha mafanikio ya mageuzi ya kilimo, hali ambayo inaweza kuathiri juhudi za kuboresha usalama wa chakula na kusaidia wakulima wadogo," ripoti inaongeza.
Lengo kuu la nguzo ya kilimo lilikuwa kuboresha uzalishaji wa kilimo ili kuhakikisha utoshelevu wa chakula nchini, kuunda ajira na kuongeza mauzo ya nje ya Kenya.
Katika mipango ya BETA, serikali ya Kenya Kwanza pia ilikuwa imepatia kipaumbele viwanda katika kila kaunti, kwa lengo kuu la kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji kupitia viwanda vya usindikaji wa mazao ya kilimo.
Hata hivyo, Bi Nancy Gathungu anasema katika ripoti yake kwamba kaunti zinakabiliwa na changamoto za kifedha katika kutekeleza mradi huu kutokana na kucheleweshwa kwa mgao wa fedha kutoka kwa serikali kuu.
Kwa mfano, katika mwaka wa kifedha wa 2023/2024, serikali ilitenga Sh4.5 bilioni kwa kaunti 18 ili kuanzisha maeneo ya viwanda, lakini ilitoa Sh1.52 bilioni pekee, ikisababisha pengo la Sh3.48 bilioni.
[caption id="attachment_165242" align="alignnone" width="300"] Makao makuu ya bima ya afya ya SHIF. PICHA|MAKTABA[/caption]"Hii inamaanisha kuwa kaunti zinakabiliwa na changamoto za kukamilisha ujenzi wa maeneo hayo, jambo ambalo litachelewesha zaidi utekelezaji wake na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa," anasema Bi Gathungu.
"Masuala makubwa kama vile mikopo isiyolipwa kwa kiwango cha juu na tofauti katika mgao wa fedha huathiri biashara ndogo. Aidha, kuna wasiwasi kuhusu vigezo vinavyotumiwa kusambaza fedha, hali ambayo imeleta dosari na usimamizi mbaya ambao unaweza kuzuia ukuaji wa biashara hizi na uendelevu wake," ripoti inasema.
Bi Gathungu anasema masuala kama vile upungufu wa fedha, taratibu tata za ununuzi, mipango duni, usimamizi mbaya wa fedha, na migogoro kuhusu umiliki wa ardhi zinaweza kuchelewesha mipango hiyo.
"Mpango huu unaweza kushindwa kufanikisha lengo la kujenga nyumba 200,000 kwa mwaka, hivyo kuchelewesha utekelezaji wa ajenda ya makazi na mchango wake katika mageuzi ya kiuchumi," inasema ripoti hiyo.
Bi Gathungu anasema kuna haja ya mageuzi ya haraka na uwekezaji wa kimkakati katika sekta ya afya ili kuhakikisha mpango huu unafanikishwa.
Anasema licha ya kutengwa kwa Sh204.5 bilioni na kuanzishwa kwa Bima ya Afya ya Jamii (SHIF) unaokadiriwa kuwafikia wananchi milioni 15, bado kuna changamoto nyingi katika sekta hii.