Gachagua: Hatutataja mapema mgombeaji wa kung’oa Ruto, kuepuka kuhujumiwa

WAKENYA watalazimika kusubiri zaidi ya mwaka mmoja ili kujua mgombeaji urais wa upinzani atakayekabiliana na Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua alisema Jumanne, huku akipuuzilia mbali madai ya migawanyiko katika upinzani.
Akihutubia waombolezaji katika mazishi ya Mchungaji Joseph Nzola wa kanisa la Jesus Celebration Centre eneo la Katelembo, Kaunti ya Machakos, Bw Gachagua alimlaumu Rais William Ruto kwa kupanga njama ya kugawanya upinzani kwa kuchochea migawanyiko miongoni mwa viongozi wa upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Hata hivyo, alionyesha matumaini kuwa upinzani utasalia kuungana na utafanikiwa kumuondoa Rais Ruto mamlakani.
“Tumesikiliza Wakenya wakisema tunapaswa kuketi pamoja na kupanga namna ya kuleta serikali mpya. Tunashughulikia hilo. Bw Musyoka, Eugene Wamalwa, George Natembeya, Fred Matiang’i na Riggy G ambaye yuko katikati ya mazungumzo haya. Nataka kuwahakikishia Wakenya kwamba tuna mpango wa kuwaletea uongozi bora. Wanajaribu kutugawanya ili kila mmoja aende kivyake lakini sisi si wajinga. Tutabaki pamoja,” alisema.
“Wakenya wanapaswa kujua kuwa sisi ni wazalendo na hivyo tutafanya kilicho sawa. Tutaweka kando maslahi ya kibinafsi kwa ajili ya nchi hii. Tutachelewesha kutangaza mpango wetu wa kugawana mamlaka hadi Desemba 2026. Tukitangaza mapema, watatuhujumu,” aliongeza Bw Gachagua huku akiwaongoza waombolezaji kumkosoa Rais Ruto kwa utawala mbaya.
Kauli za Bw Gachagua zinajiri wakati ambapo kumekuwa na tetesi kuwa upinzani umegawanyika. Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni alichochea mjadala huo hivi majuzi baada ya kutangaza kuwa chama hicho kinaunga mkono azma ya urais ya Bw Matiang’i.
Baadhi ya wandani wa Bw Matiang’i wamekuwa wakimtaka kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka kusitisha ndoto yake ya kuwania urais mwaka 2027 na badala yake amuunge mkono Bw Matiang’i.
Bw Musyoka hakuzungumzia suala hilo katika mazishi ya Mchungaji Nzola.
Badala yake, alitumia fursa hiyo kulaani kile alichokitaja kama vitisho kutoka kwa Rais Ruto dhidi ya upinzani, akitoa mfano wa tukio ambalo wahuni walivamia kanisa la PCEA Mwiki alikohudhuria ibada Bw Gachagua.
“Kufukuzwa madarakani hakumaanishi kwamba usihudhurie ibada. Kile kilichotokea kanisani Mwiki kinaweza kugeuka kuwa mauaji. Acheni vitisho,” alisema.
Aliwataka viongozi wa makanisa kuunga mkono upinzani katika kumkemea Rais Ruto ambaye amekuwa akimshutumu kwa uongozi mbaya.
“Tusimwache Gachagua awe msema kweli pekee. Kanisa linapaswa kusimama na ukweli. Ninyi ni chumvi ya dunia,” alisema.
Makamu wa Rais wa zamani akielekeza maneno kwa wachungaji wa kipentekoste waliokuwepo.