Gachagua aiga Ruto akijivumisha kitaifa

ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua anaonekana kutumia mkakati sawa na ule Rais William Ruto alitumia kumkabili Rais Uhuru Kenyatta kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.
Gachagua anapanga kutangaza chama cha kisiasa Mei 15, hatua ambayo inaweza kumnyima Ruto uungwaji mkono eneo la Mlima Kenya kuelekea 2027.
Rais Ruto alianzisha chama cha United Democratic Alliance (UDA) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, huku akiendelea kuwa naibu kiongozi wa chama cha Jubilee chini ya Rais Kenyatta.
Alifanikiwa kuwaunganisha viongozi waliokuwa madarakani chini ya UDA, bila kutangaza kujiondoa rasmi Jubilee ili kuepuka adhabu ya chama.
Mpango huo ulifaulu, akashinda urais dhidi ya Raila Odinga aliyeungwa mkono na Kenyatta.Sasa akiwa katikati ya muhula wake wa kwanza, Rais Ruto anakabiliwa na hali kama ile aliyowahi kutumia, huku wapinzani wake wakisema ni “kisasi cha kisiasa”, kwani Gachagua, ambaye aliondolewa madarakani Oktoba 2024, tayari anapata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya viongozi wa UDA wanaotarajiwa kujiunga na chama chake.
“Mnamo 2013, Ruto alimtatiza mkubwa wake lakini hakufutwa kazi. Kenyatta alimvumilia hadi baada ya muhula wa pili ndipo akamkabili. Ruto alidhani yeye ni mjanja zaidi. Sasa alipokutana na naibu ‘sumu’ kama Gachagua, alimhukumu mara moja,” asema mwanasiasa na mtaalamu wa siasa, John Okumu.
Kama vile Ruto alivyokuwa na kikundi kidogo alipoanza UDA, Gachagua pia ana kundi dogo la wanasiasa wanaomuunga mkono, lakini anatarajia wengi zaidi kumfuata uchaguzi utakavyokaribia.
“Ndio maana hatima za kisiasa za Ruto na Gachagua zinafanana. Wanakaribia kugongana katika mapambano makali ya kuwavuta viongozi na kuunda miungano ya maeneo,” asema mhadhiri Charles Mwangi kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta.
Anasema: “Ruto alijenga UDA akiwa bado ofisini, Gachagua anafanya hivyo akiwa ameondolewa madarakani. Ruto alikuwa na taarifa za kijasusi, Gachagua anafanya hivyo akiwa jangwani.”
Lakini, jambo kuu la kuamua hatima yao linabaki kuwa kura za Mlima Kenya.“Ruto alijipanga vilivyo Mlima Kenya 2022, akauvuta upande wake, na wakamkataa mwana wao Kenyatta. Mlima Kenya ulimfanya Ruto kuwa rais,” asema mchambuzi wa siasa Gasper Odhiambo.
Gachagua anaonekana kupanga kumfanyia Ruto kile Ruto alimfanyia Kenyatta — kumnyima uungwaji mkono wa Mlima Kenya.“Ruto bado anatumia ahadi za maendeleo kama silaha yake kuu. Lakini hata Kenyatta alipotekeleza maendeleo makubwa, wapiga kura wa Mlima Kenya walimpuuza na kumuunga mkono Ruto,” asema Odhiambo.
“Ruto sasa anawahimiza watu wa Mlima Kenya wapuuze ukabila, kama alivyofanya Kenyatta, lakini inaonekana hadithi hiyo inajirudia.”Tatizo lingine ambalo Ruto anakumbana nalo kama Kenyatta ni jinsi ya kuunganisha maeneo mengine.
Profesa Peter Kagwanja anasema hali hii ndiyo ilipelekea maridhiano kati ya Kenyatta na Odinga mnamo 2018, kwa sababu Odinga alikuwa na ufuasi wa takribani asilimia 50 ya nchi.
“Sasa Ruto pia ana hali sawa na Odinga,” anasema.Anasema Rais Ruto pia alikutana na Kenyatta huko Ichaweri mnamo Desemba, baada ya kumleta Odinga kwenye serikali, kwa lengo la kumdhibiti Gachagua na kuzuia Mlima Kenya kumponyoka.
Kama vile Odinga alivyokuwa chanzo cha mzozo kati ya Kenyatta na Ruto, sasa tena ndiye aliyesaidia kuondolewa kwa Gachagua.Agosti 5, 2020, wabunge 135 walitangaza kuhamia UDA wakisema Jubilee imekufa.
Leo, Gachagua pia ameungana na wachache wakisema UDA imekufa, na kwamba chama kipya kinahitajika.Kama vile Ruto alivyojenga miungano yake kwa kuwaleta Mudavadi, Wetang’ula, Mutua, Kingi, Muturi na wengine, Gachagua pia anafanya vivyo hivyo — akifanya mazungumzo na Kalonzo Musyoka, Eugene Wamalwa, Fred Matiang’i, Kipruto Kirwa na George Natembeya.
Cecily Mbarire, aliyekuwa mbunge mteule wa Jubilee aliyebaki na Ruto, sasa ndiye mwenyekiti wa UDA na anasema chama hicho kiko imara kuelekea 2027.Lakini Gachagua anaendeleza msimamo kuwa UDA imekufa, sawa na Ruto alivyofanya kwa Jubilee.“UDA iko wapi? Tayari imemezwa na ODM.
ANC ya Mudavadi nayo imekufa. Hakuna chama kinachoongoza,” alisema Gachagua Jumapili iliyopita.Hata hivyo, Bi Mbarire anasema UDA inajiimarisha kupitia uchaguzi wa mashinani.