Dk Mwinyi kuwazadia Simba Sh Mil.267

Habari Leo
Published: May 25, 2025 09:12:48 EAT   |  Sports

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kutoa dola 100,000 za Marekani (Sh Mil.267) kwa wachezaji wa Simba kama wakitwaa Kombe la Shirikisho Afrika leo. Dk Mwinyi alitoa ahadi hiyo usiku wa kuamkia leo, alipokutana na wachezaji wa Simba kwenye kambi yao, ikiwa ni maandalizi ya fainali …

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kutoa dola 100,000 za Marekani (Sh Mil.267) kwa wachezaji wa Simba kama wakitwaa Kombe la Shirikisho Afrika leo.

Dk Mwinyi alitoa ahadi hiyo usiku wa kuamkia leo, alipokutana na wachezaji wa Simba kwenye kambi yao, ikiwa ni maandalizi ya fainali yao na RS Berkane itakayofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Amewatakia mchezo mwema na kuwaeleza umuhimu wa kushinda na kueleza kuwa serikali inatoa ushirikiano wa kila namna kuhakikisha wanafanya vizuri.