Dk Mwinyi aagiza nyumba hifadhi ya barabara zivunjwe

Habari Leo
Published: Jan 09, 2025 04:48:02 EAT   |  Travel

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na…

The post Dk Mwinyi aagiza nyumba hifadhi ya barabara zivunjwe appeared first on HabariLeo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kuondoa nyumba zilizokuwepo barabarani na kuacha wazi hifadhi ya barabara.

Rais Mwinyi alitoa tamko hilo jana alipozindua barabara za kilometa 10 za Micheweni – Kiuyu-Maziwa Ng’ombe na Barabara ya Michweni -Shumba Mjini hadi Bandarini Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Dk Mwinyi alisema kumekuwa na tabia ya watu kujenga pembezoni mwa barabara kwa kutegemea kulipwa fidia na serikali, jambo ambalo si sahihi.

Rais Mwinyi alizitaka halmashauri kusimamia suala hilo na kudhibiti utoaji wa vibali holela vya ujenzi pembezoni mwa barabara.

Aliwahimiza wananchi kuacha kujenga katika hifa dhi za barabara kwani zim etengwa maalumu kwa ajili ya kuendeleza miundombinu mingine. Aliwahakikishia wanan chi wa Pemba kuwa barabara nyingi kisiwani humo zitajengwa kwa kiwango cha lami.

Alisema serikali ina programu maalumu ya kuziwekea taa barabara zote zilizojengwa kwa kiwango cha lami nchi nzima.

“Hatuwezi kujenga barabara kiwango cha lami halafu taa zitushinde,” alisema.

Alisisitiza kuwa barabara zilizofikia ujenzi wa kuwe kwa kifusi zikiwa barabara kuu au zile za ndani zote zitawekwa lami.

Akizungumzia bei za chakula, Dk Mwinyi alisema serikali imeamua kuzijenga bandari za Mkoani, Shumba Mjini na Mkoani ili bidhaa zinazotoka nchi za nje zipele kwe moja kwa moja Pemba hatua itakayopunguza gharama za usafirishaji.

Rais Mwinyi amesisitiza kuwa itamkabidhi mkanda rasi aliyejenga Bandari ya Mkoani, Bandari za Shumba Mjini na Wete ili aanze ujenzi hivi karibuni ili kufikia lengo hilo.

Aidha, Rais Mwinyi ame wathibitishia wananchi kuwa serikali itaikabidhi Kampuni ya IRIS iliyojenga barabara zilizozinduliwa za Michewe ni kazi ya kuziunganisha na barabara kuu na ndogo.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa barabara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Habiba Hassan alisema ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa kilometa 10 ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020/2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar, Mpango Mkuu wa Maende leo wa Taifa na Mpango Mkuu wa Usafiri ambao barabara zenye kilometa 140.9 zimejengwa Unguja na kilometa 134.9 zimejengwa Pemba

The post Dk Mwinyi aagiza nyumba hifadhi ya barabara zivunjwe appeared first on HabariLeo.