Dk. Mwilike aishauri serikali kuongeza idadi ya wakunga

DAR-ES-SALAAM: RAIS wa Chama cha Wakunga Tanzania, Dk. Beatrice Mwilike, ameishauri serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuongeza…
The post Dk. Mwilike aishauri serikali kuongeza idadi ya wakunga appeared first on HabariLeo.
DAR-ES-SALAAM: RAIS wa Chama cha Wakunga Tanzania, Dk. Beatrice Mwilike, ameishauri serikali kwa kushirikiana na wadau wengine kuongeza idadi ya wakunga nchini ili kupunguza vifo vya uzazi.
Akizungumza jijini Dar-es-salaam na Dailynews Digital katika mahojiano maalum, Dk. Mwilike amesema jamii imekuwa ikiwanyooshea vidole wakunga kwa kusababisha vifo vya uzazi, lakini ukweli ni kwamba bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa watendaji katika sekta hiyo.
“Tumekuwa tukishuhudia ongezeko la vifo vya uzazi, na licha ya juhudi za serikali, bado tunahitaji kuongeza idadi ya wakunga ili kukabiliana na hali hii. Wakunga wengi wanakabiliwa na uzito wa kazi na uhaba wa rasilimali,” alisema Dk. Mwilike.
Aidha, Dk. Mwilike alifafanua kuwa sekta ya ukunga inachukuliwa kama sekta ya kijadi, ambapo kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ya kuwa na wataalamu wengi wa ukunga wanaopatiwa mafunzo kitaalamu.
“Ni muhimu kwa wakunga kuwa na ujuzi na maarifa yanayohitajika ili kuwahudumia kina mama na watoto kwa usalama,” aliongeza.
Dk. Mwilike alisema kuwa ushirikiano baina ya serikali, wadau wa afya, na jamii ni muhimu ili kuboresha huduma za uzazi na kuhakikisha kuwa kila mama anapata huduma bora wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua.
SOMA: Tanzania, China kuwanoa wakunga
The post Dk. Mwilike aishauri serikali kuongeza idadi ya wakunga appeared first on HabariLeo.