Dk. Mwigulu – Jiungeni soko la hisa la DSM

Habari Leo
Published: Jan 24, 2025 14:25:03 EAT   |  Business

DAR-ES-SALAAM: WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Benki ya Azania kwa kuorodheshwa rasmi katika Soko la Hisa…

The post Dk. Mwigulu – Jiungeni soko la hisa la DSM appeared first on HabariLeo.

DAR-ES-SALAAM: WAZIRI wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, ameipongeza Benki ya Azania kwa kuorodheshwa rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Akizungumza katika ofisi za makao makuu ya soko la hisa jijini Dar es Salaam leo, tarehe 24 Januari 2025, Dk. Mwigulu alisema ni muhimu kwa taasisi nyingine za fedha kuiga mfano mzuri wa Benki ya Azania.

Alisisitiza kuwa ni muda wa kuhamia kwenye uchumi wa kisasa, ukiacha utegemezi wa fedha taslimu na kuelekea kwenye uchumi wa “cashless.”

“Hatuna namna, lazima twende na wakati kutoka kwenye uchumi wa kutoa cash kwenda kwenye uchumi usio na cashless,” alisema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo aliongeza kuwa maendeleo haya yanaendana na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amesaidia kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

“Hawezi kuwa na nchi kubwa kama hii inayotekeleza miradi ambayo hata nchi zilizoendelea hazijaweza kutekeleza, na bado kuendelea kuwa na uchumi wa kizamani kama ilivyo katika hadithi za God Must Be Crazy. Lazima tubadilike, majira yanatutaka tuwe hivi,” aliongeza.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Esther Mang’enya, alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa benki kuimarisha uwekezaji katika soko la hisa.

“Tunashukuru, tangu kuuza hisa zetu tumepata faida kubwa ya zaidi ya asilimia 210, sawa na shilingi bilioni 63.3. Hii ni faraja, tunashukuru sana,” alisema Mang’enya.

Benki hiyo pia imepanga kutumia faida ya uwekezaji huo wa tija kusaidia makundi maalum kama wanawake, vijana, na wajasiriamali wadogo. SOMA: Tanzania yaingia soko la hisa New York

 

The post Dk. Mwigulu – Jiungeni soko la hisa la DSM appeared first on HabariLeo.