DC Mwanziva ataka ubora barabara ya Mtange – Kineng’ene
MKUU wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva ameuagiza Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Lindi…
The post DC Mwanziva ataka ubora barabara ya Mtange – Kineng’ene appeared first on HabariLeo.
MKUU wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva ameuagiza Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Lindi kusimamia ubora wa ujenzi wa barabara ya Mtange – Kineng’ene yenye urefu wa mita 600 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
DC Mwanziva amesema hayo alipokuwa akziungumza na wanahabari katika ziara yake ya kukagua mradi huo unaojengwa kwa zaidi ya Sh milioni 400 Wilaya ya Lindi.
Aidha, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mradi huo.
“Nilipata nafasi ya kugusia namna ambavyo serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya matengenezo na maboresho ya Barabara Katika Wilaya ya Lindi, ambapo kwa sasa bajeti imeongezeka kutoka wastani wa bilioni mbili kwa mwaka hadi kufikia bilioni nane kwa mwaka 2024/2025,” amesema DC Mwanziva.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Mhandisi Dawson Pascal amesema mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na umefikia 70% ya utekelezaji wake.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lindi Mjini, Asha Mwendwa amesisitiza mradi huo kukamilika kwa wakati kwani unahudumia wananchi wengi wanaoishi Kineng’ene, Milola, Matimba, Chikonji na Nangaru hivyo ni tegemeo na litazidi kuchagiza uchumi na uchukuzi kiujumla.
The post DC Mwanziva ataka ubora barabara ya Mtange – Kineng’ene appeared first on HabariLeo.