CPJ – Wanahabari 361 wafungwa Barani Afrika
Takriban wanahabari 67 wamefungwa barani Afrika, ikiwa ni sehemu ya changamoto inayoendelea ya uhuru wa vyombo vya habari.…
The post CPJ – Wanahabari 361 wafungwa Barani Afrika appeared first on HabariLeo.
Takriban wanahabari 67 wamefungwa barani Afrika, ikiwa ni sehemu ya changamoto inayoendelea ya uhuru wa vyombo vya habari.
Kesi hizi zinachangia idadi ya jumla ya wanahabari 361 waliofungwa jela duniani kufikia Disemba 1, kulingana na shirika la kutetea haki za waandishi wa habari, CPJ.
Mratibu wa programu ya CPJ barani Afrika, Muthoki Mumo, amesema ripoti hiyo inaonyesha jinsi tawala za kimabavu zinavyotumia sheria kama zana za kukandamiza waandishi wa habari kwa kutumia sheria za usalama wa taifa, kupambana na ugaidi na uhalifu wa mtandaoni.
Mumo alisema nchi kama Burundi, Ethiopia na Nigeria zinatumia sheria za usalama wa taifa kama njia ya kufanya uandishi wa habari kuwa kosa la jinai.
Nchini Nigeria, wanahabari wanne wamefungwa mashtaka chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni kwa kuripoti kuhusu ufisadi. SOMA: ICC yaombwa kuchunguza mauaji ya waandishi
Huko Ethiopia, waandishi sita wako gerezani, watano kati yao wakikabiliwa na mashtaka chini ya sheria za kupambana na ugaidi. Wanaweza kukutana na adhabu kali ikiwa watakutwa na hatia.
Kadhalika Burundi, mwandishi Sandra Muhoza wa chombo cha habari cha mtandaoni, La Nova, alihukumiwa chini ya sheria za usalama wa taifa baada ya kutuma ujumbe wa WhatsApp, akionyesha mfano mwingine wa jinsi uandishi wa habari unavyofanywa kosa la jinai.
The post CPJ – Wanahabari 361 wafungwa Barani Afrika appeared first on HabariLeo.