Changamoto za walimu kushughulikiwa

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma kimesema kuwa Samia Teachers Mobile Clinic itasaidia kumaliza changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu…
The post Changamoto za walimu kushughulikiwa appeared first on HabariLeo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma kimesema kuwa Samia Teachers Mobile Clinic itasaidia kumaliza changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu katika utendaji kazi wao na maslahi ya walimu kwa jumla.
Katibu wa CCM Mkoa Kigoma Charles Pallangyo alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa Kigoma ambapo alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati kuondoa changamoto zote zinazowakabili walimu nchini.
Katika salamu za CCM kwenye mkutano huo zilizotolewa kwa niaba yake na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo alisema kuwa serikali itaendelea kuisimamia serikali ili kuhakikisha walimu wanawekewa mazingira mazuri ya kazi lakini pia kuhakikisha stahiki za walimu zinalipwa na zinalipwa kwa wakati na kuwepo kwa Samia Teachers Mobile Clinic kunalenga kutimiza azma hiyo.
Kaimu Katibu Tawala Msaidizi mkoa Kigoma sekta ya elimu, Hamka Tambwe (katikati aliyekaa) akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa Kigoma
Akifungua mkutano huo Kaimu Katibu Tawala Msaidizi mkoa Kigoma sekta ya elimu, Hamka Tambwe alisema kuwa serikali mkoani Kigoma itaendelea kuboresha maslahi ya walimu na mazingira yao ya kazi ili waweke kufanya kazi vizuri kwa manufaa ya wanafunzi wa Tanzania.
Tambwe ambaye alikuwa akimwakilisha Katibu Tawala wa Kigoma, Hassan Rugwa amesema kuwa tayari ofisi ya Katibu Tawala mkoa Kigoma imeshawaandikia wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa Kigoma kuhakikisha wanahakiki na kulipa madeni yote ya walimu na kuandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu kukumbushia madeni hayo ili kuhakikisha madeni yote yanakwisha.
Walimu wajumbe wa mkutano nkuu wa CWT mkoa Kigoma wakiwa kwe ye mkutano
Awali akitoa taarifa ya hali ya utendaji wa walimu mkoa Kigoma Katibu wa CWT mkoa Kigoma, Cassioano Mbajije alisema kuwa chama hicho kimefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi uliopo madarakani ikiwemo kusimamia kesi za walimu na kufanya ziara mbalimbali za kuimarisha utendaji wa chama hicho.
Sambamba na hilo Katibu huyo wa CWT mkoa Kigoma alisema kuwa Samia Teachers Mobile Clinic iliyoanzishwa na chama hicho itazaa matunda na kuleta mustakabali mzuri kwa walimu lakini wakiomba pia Halmashauri zitumie mapato ya ndani kulipa madeni na stahiki za walimu.
The post Changamoto za walimu kushughulikiwa appeared first on HabariLeo.