‘Bulldozer’ lagonga nyumba na kujeruhi watano Geita

Habari Leo
Published: Apr 03, 2025 15:33:15 EAT   |  General

WATU watano wamejuruhiwa baada ya mtambo (Bulldozer) mali ya mgodi wa Bucreef kuacha njia na kugonga nyumba za…

The post ‘Bulldozer’ lagonga nyumba na kujeruhi watano Geita appeared first on HabariLeo.

WATU watano wamejuruhiwa baada ya mtambo (Bulldozer) mali ya mgodi wa Bucreef kuacha njia na kugonga nyumba za makazi katika kitongoji cha Isingilo kijiji cha Lwamugasa wilayani Geita.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwamugasa, Mwita Amos ameeleza tukio hilo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya na kueleza ajali ilitokea majira ya saa nane usiku wa kuamukia Aprili 3, 2025.

Mwita amesema kaya tatu zimeathiriwa na tukio hilo ambalo limepelekea majeruhi watano waliofikishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita na wengine kulazwa katika kituo cha Afya Katoro.

Amesema taarifa zinaeleza mtambo huo maarufu kama Bulldozer’ lilitokea kwenye mgodi wa Bucreef na lilipita bila kuwa na mwendeshaji ndaji yake na kupelekea uharibifu kwenye makazi ya watu.

Mmoja wa manusura wa ajali hiyo, Athuman Charles amesema kabla ya tukio walisikia muungurumo wa kitu kinapita, lakini kwa sababu wanaishi karibu na mgodi walihisi ni mitambo ya mgodi.

“Ghafla tulisikia kama kuna kitu kinadondoka, tukasikia kuna watu wanalia, kuna mzee alikuwa anapiga yowe kuja kuangalia kumbe kuna nyumba imedondoka kwenye nyumba iliyokuwa na watoto sita” amesema Athuman.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya, Hashimu Komba amethibitisha tukio hilo na kueleza uchunguzi unaendelea ili kubaini kiini na chanzo halisi cha ajali.

Amesema taarifa za awali zinaeleza dreva wa mtambo huo alikuwa akijihusisha na wizi wa mafuta na alikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wananunua mafuta ambao wawili tayari wameshakamatwa.

Amesema baada ya walinzi wa mgodi kubaini kuna wizi unaendelea, walianza kumfuatilia mwendeshaji wa mtambo aliondoka eneo la tukio, alipobaini ufuatiliaji unaendelea, aliruka na kutelekeza mtambo.

“Sasa mitambo hii ina uwezo wa kujiendesha yenyewe, ukiliwasha unaweza ukatoa funguo na likaendelea, ndiyo maana kwa mashuhuda mliowahi mmelikuta linaendelea kuunguruma eneo la tukio”, amesema Komba.

The post ‘Bulldozer’ lagonga nyumba na kujeruhi watano Geita appeared first on HabariLeo.