BSS kufanyika Februari 28 Dar es Salaam

DAR ES SALAAAM: FAINALI ya shindano la kusaka vipaji nchini, Bongo Star Search (BSS), msimu wa 15, inatarajiwa…
The post BSS kufanyika Februari 28 Dar es Salaam appeared first on HabariLeo.
DAR ES SALAAAM: FAINALI ya shindano la kusaka vipaji nchini, Bongo Star Search (BSS), msimu wa 15, inatarajiwa kufanyika Februari 28, 2025, katika ukumbi wa Ware House, Masaki jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa kwanza wa mashindano hayo ataondoka na kitita cha Sh milioni 20, huku mshindi wa pili akipata milioni 3, na wa tatu akijinyakulia milioni 1.
Akizungumza na HabariLeo, Dar es Salaam, Jaji Mkuu na Mkurugenzi wa Benchmark, Madam Rita Paulsen, amesema kuwa fainali ya mwaka huu itakuwa ya kipekee kwani inajumuisha washiriki sita kutoka mataifa matatu—Tanzania, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
SOMA ZAIDI: Fainali za BSS kufanyika Feb. 4
“Msimu huu umekuwa wa kipekee ukilinganisha na mingine yote iliyopita. Sasa tumevuka mipaka na kujumuisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika. Haikuwa kazi rahisi kufikia hapa, kwani ushindani ulikuwa mkubwa na vipaji vilikuwa vingi. Hata hivyo, sasa tunaelekea kwenye fainali ambapo tutapata mshindi wa msimu huu,” amesema Madam Rita.
Katika hatua nyingine, msanii Abiudi amejitoa kwenye mashindano hayo, ambapo Madam Rita alifafanua kuwa alijitoa mwenyewe kutokana na sababu binafsi zinazohusiana na mahusiano yake ya kimapenzi.
Aidha, alisisitiza kuwa lengo la BSS ni kuwawezesha wasanii wachanga kujulikana zaidi kwenye jamii na kuwa mastaa wanaojipatia kipato kupitia sanaa zao. Aliwataka wadau kuunga mkono mashindano haya kwa kufika kwenye fainali na kusaidia kumpata mshindi wa mwaka huu.
Viingilio kawaida ni Sh 20000 VIP Sh 30000 na VVIP ni Sh 50000 na Vabe 15 ni Sh laki moja.
The post BSS kufanyika Februari 28 Dar es Salaam appeared first on HabariLeo.