Biteko ataja mambo 7 kukuza afya, ustawi wenye ulemavu

Habari Leo
Published: Jan 25, 2025 08:39:20 EAT   |  News

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaja mambo saba ambayo serikali inafanya kukuza afya…

The post Biteko ataja mambo 7 kukuza afya, ustawi wenye ulemavu appeared first on HabariLeo.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ametaja mambo saba ambayo serikali inafanya kukuza afya na ustawi wa watu wenye ulemavu nchini.

Dk Biteko alitaja mambo hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa vya kinga na uchunguzi wa saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino iliyoandaliwa na Mkurugenzi wa Manara Foundation na Manara Tv,
Haji Manara.

Alisema serikali imeweka mipango ya kukuza afya na ustawi wa watu wenye ualbino kwa kuimarisha huduma za afya, ikiwa ni pamoja na kuzindua Mpango Kazi wa Taifa kwa Ustawi wa Watu Wenye Ualbino.

“Mpango huu niliuzindua mimi mwenyewe Desemba 3, mwaka jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hapa
Dar es Salaam, mpango huu umeainisha afua mahususi za kinga ya saratani ya ngozi kwa watu wenye ualbino’’ alisema.

SOMA: ‘Tutaendelea kusimamia ustawi wenye ualbino’

Alisema pia, serikali imezindua mkakati wa taifa wa Teknolojia saidizi 2024/2027 pamoja na kujenga vituo vya kutolea huduma za afya vyenye miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu, ikiwemo wenye ualbino.

“Hadi kufikia Machi 2024 kulikuwa na vituo vya afya 12,266 vyenye miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu,” alisema.

Alisema Novemba 2024 serikali ilitoa Sh bilioni nne kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kwa ajili ya ununuzi wa vifaa saidizi ikiwemo kofia pana, miwani, lenzi za kusomea pamoja na kuandaa mfumo wa kielektroniki wa kukusanya taarifa na takwimu za watu wenye ulemavu.

“Mfumo huu unawezesha kuwatambua na kuwasajili watu wenye mahitaji mbalimbali, ikiwemo wenye ualbino na kujua wapi tunapaswa kupeleka rasilimali kwa ajili ya kuwahudumia,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Ualbino Tanzania (TAS), Godson Mollel aliomba serikali kupitia Ofisi ya Hazina kupeleka ruzuku kwa vyama vya watu wenye ulemavu pamoja na haki kutendeka kwa kiongozi wa dini anayetuhumiwa kuhusika na mauji ya mtoto, Asimwe mkoani Kagera.

Aidha, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa vifaa vya kisasa vya kupima saratani katika Taasisi ya
Saratani Ocean Road.

“Leo Ocean Road kuna kifaa cha kugundua saratani tuliyonayo, ukigundulika una saratani unapata matibabu, maisha yetu sasa yatakuwa marefu,” alisema.

The post Biteko ataja mambo 7 kukuza afya, ustawi wenye ulemavu appeared first on HabariLeo.