Bilioni 518 kuendeleza elimu Zanzibar
PEMBA : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza bajeti ya Maendeleo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Sh.bilioni 83.2 mwaka 2021/22 hadi kufikia Sh.bilioni 518 mwaka 2024/2025. Akifungua shule mpya ya sekondari ya Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa …
The post Bilioni 518 kuendeleza elimu Zanzibar first appeared on HabariLeo.
PEMBA : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza bajeti ya Maendeleo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kutoka Sh.bilioni 83.2 mwaka 2021/22 hadi kufikia Sh.bilioni 518 mwaka 2024/2025.
Akifungua shule mpya ya sekondari ya Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini, Pemba ikiwa ni mwendelezo wa kupongeza miaka minne ya mafanikio ya serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk.Mwinyi.
Aidha amesema bajeti hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 522.6 ambayo Imesaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi mingi ya kimkakati, inayolenga kuboresha elimu ya watoto na kuweka misingi imara ya maendeleo ya muda mrefu kwa Taifa.
Akizungumzia kuhusu bajeti ya elimu ya juu, Rais Dk. Mwinyi amesema serikali imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu kutoka TZS bilioni 11.5 kwa mwaka 2021/2022 hadi bilioni 33.4 mwaka 2024/2025 bajeti iliyoongeza idadi ya wanafunzi kutoka 4289 hadi kufikia 6,060.
Rais Dk. Mwinyi amesema hadi sasa Serikali tayari imejenga madarasa 2,773 sawa na zaidi ya asilimia 184 ya shabaha ya madarasa 1,500 yaliyoelekezwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, yenye uwezo wa kuchukua wastani wa wanafunzi 45 kwa kila awamu.
SOMA : SMZ kuendelea kuifungua Pemba
The post Bilioni 518 kuendeleza elimu Zanzibar first appeared on HabariLeo.