Bil 5/- zajenga kitengo cha tiba mionzi KCMC

Habari Leo
Published: Mar 03, 2025 06:30:53 EAT   |  News

SERIKALI imewekeza Sh bilioni tano za kujenga jengo la kituo cha tiba mionzi na ununuzi wa vifaatiba katika…

The post Bil 5/- zajenga kitengo cha tiba mionzi KCMC appeared first on HabariLeo.

SERIKALI imewekeza Sh bilioni tano za kujenga jengo la kituo cha tiba mionzi na ununuzi wa vifaatiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Kaskazini (KCMC) mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama alisema hayo mjini Moshi juzi alipofanya ziara katika hospitali ya KCMC ili kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo linalotoa huduma za saratani kwa njia ya tiba mionzi.

Jenista alisema ameridhishwa na ujenzi wa kituo hicho cha tiba mionzi ambacho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma hizo mwezi ujao.

“Sekta ya afya sisi sio washindani, tunashirikiana pamoja ili kuhakikisha tunatoa hudumu za afya zilizo bora kwa wananchi na kuwafikia wananchi wote,” alisema.

Jenista alisema kituo hicho kitakuwa ni kati ya vituo vichache ambavyo vinatoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa njia ya mionzi.

Alisema kituo hicho kitakuwa na wataalamu wenye ubobezi na umahiri wa hali ya juu na wasomi kwa kufadhiliwa na serikali.

Jenista alihimiza umuhimu wa kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kuepuka matumizi ya mafuta mengi, sukari na chumvi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

“Tumekubaliana kama serikali tutaendelea na kampeni ya hali ya juu kwa kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanatumia muda mrefu kwenye matibabu, fedha nyingi katika kuyatibu lakini pia yanahitaji uwekezaji mkubwa ambao utawezesha huduma hizi kutolewa inavyotakiwa,” alisema.

Jenista alihimiza wananchi waendelee kuelimishana kuhusu magonjwa ya milipuko na wachukue tahadhari.

The post Bil 5/- zajenga kitengo cha tiba mionzi KCMC appeared first on HabariLeo.