Bil 143/- waingiziwa wakulima wa korosho

Habari Leo
Published: Oct 17, 2024 12:32:27 EAT   |  Business

WAKULIMA wa Korosho Mkoa wa Mtwara na Lindi wameingiza kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 143 fedha iliyotokana na mauzo ya tani 33,391,375 za korosho ghafi katika minada minne ya awamu inayoendeshwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) katika msimu wa mauzo mwaka 2024/2025. Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko hilo la Bidhaa …

The post Bil 143/- waingiziwa wakulima wa korosho first appeared on HabariLeo.

WAKULIMA wa Korosho Mkoa wa Mtwara na Lindi wameingiza kiasi cha zaidi ya Sh bilioni 143 fedha iliyotokana na mauzo ya tani 33,391,375 za korosho ghafi katika minada minne ya awamu inayoendeshwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) katika msimu wa mauzo mwaka 2024/2025.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko hilo la Bidhaa Tanzania TMX,  Godfrey Malekano amesema mpaka sasa kiasi cha fedha zaidi ya Sh bilioni 143 kimepatikana katika minada minne ya korosho iliyofanyika katika mikoa wa Lindi na Mtwara.

Amesema katika tani hizo za korosho, Mkoa wa Lindi ulipeleka sokoni jumla ya tani 11,454,260 za korosho ghafi zenye thamani zaidi ya Sh bilioni 48.9 ambapo minada yake imefanyika Oktoba 12 hadi 13 2024.

Haya hivyo Mkoa wa Mtwara umepeleka sokoni jumla ya tani 21,937,115 za korosho ghafi zenye thamani zaidi ya Sh bilioni 94.2  na kuuzwa katika minada ya Oktoba 11 hadi 14  mwaka huu katika msimu huo wa mauzo.

Aidha, Mtendaji Mkuu huyo  ameendelea kuwaomba wakulima wa korosho kuendelea kupeleka sokoni korosho zenye ubora ili waweze kuendana na soko kwani bei nzuri sokoni inatokana na ubora wa bidhaa husika.

“Tukiwa tunaendelea na minada niendelee kuwaomba wakulima wa korosho kuendelea kupeleka sokoni korosho zenye ubora ili waweze kuendana na soko kwani bei nzuri sokoni inatokana na ubora wa bidhaa husika”amesema Malekano

Aidha minada hiyo ya korosho katika msimu wa kilimo mwaka 2024/ 2025 imeanza rasmi Oktoba 11, mwaka huu katika halmashauri ya mji Newala mkoani Mtwara.

The post Bil 143/- waingiziwa wakulima wa korosho first appeared on HabariLeo.