Bil 106/- zatekeleza miradi Bukoba Vijijini kwa miaka minne

SERIKALI imetoa Sh bilioni 106.4 kufanikisha miradi ya maji, afya, barabara, umeme na elimu katika jimbo la Bukoba…
The post Bil 106/- zatekeleza miradi Bukoba Vijijini kwa miaka minne appeared first on HabariLeo.
SERIKALI imetoa Sh bilioni 106.4 kufanikisha miradi ya maji, afya, barabara, umeme na elimu katika jimbo la Bukoba Vijijini mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka minne, Mbunge wa jimbo hilo, Jassoni Rweikiza anasema.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, mbunge huyo amesema kwa miaka minne vijiji 46 vimepata maji na miradi ya maji 38 imetekelezwa kwa gharama ya Sh bilioni 25.
Amesema mradi wa maji wa kemondo – Kanyangereko nao utatakelezwa kadri serikali inavyoleta fedha.
Amesema serikali imefikisha umeme katika vijiji vyote 94 na vitongoji 216 kati ya vitongoji 515 vimepata umeme, madarasa 62 na vyoo 238 vimejengwa, shule mpya tano bweni moja, nyumba mpya za walimu 14 na shule kongwe zikikarabatiwa kwa ufanisi wa hali ya juu.
Ameeleza kuwa anaendelea kukamilisha ujenzi wa ofisi nzuri ya CCM na anaamini kuwa atakamilisha ujenzi huo wa jengo la kisasa ifikapo Juni mwishoni mwaka huu.
Amesema changamoto kubwa kwa sasa kuwa ni wakulima wa Bukoba Vijijini ambao wakulima zao la Vannila na mpaka leo hawajawai kulipwa fedha zao huku kupitia kwa makamu huyo akiomba wakulima hao walipwe na ombi lake lingine alimuomba makamu huyo amuombe Waziri wa Fedha alete fedha za Kukamilisha mradi wa maji wa kemondo Kanyangereko utakaohudumia kata tano za jimbo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amempongeza mbunge wa Bukoba Vijijini kwa kujenga jengo la kisasa la CCM la Wilaya, pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo amewaambia wananchi kuwa moja ya jukumu kubwa la mbunge ni kusikiliza kero zao na kuzifikisha serikalini na kufatilia miradi ya maendeleo ambapo amedai kuwa mbunge mabaye asikilizi kero za wananchi afai kuchaguliwa katika uchaguzi huu.
Amesema kuwa serikali itaendelea kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kila wilaya ili kuendelea kutoa uzoefu kwa vijana wengi Mkoa wa Kagera kuendelea kujiajili na kuajiliwa huku akiwataka viongozi waliopewa dhamana na wananchi wao kuendelea kufanya ubunifu wa kuwangunisha katika mifumo ya kuwapatia vijana Pesa ya haraka kama mifugo na uvuvi.
“Natambua mkoa wa Kagera mnazungukwa na ziwa na mito mikubwa hivyo vijana wanaweza kufanya ufugaji wa Samaki wa vizimba , na ufugaji huo unaweza kuwaingizia fedha za haraka,lakini pia kama familia zinaweza kufanya ufugaji wa ng,ombe Kila kaya Hata ngombo wawili hizo familia zikawa na uhakika wa kupata maziwa na kikawepo kiwanda Cha maziwa familia zinaweza kupata pesa na kujiokoa na umasikini “Amesema Wasira
The post Bil 106/- zatekeleza miradi Bukoba Vijijini kwa miaka minne appeared first on HabariLeo.