Biashara saa 24 kuanza Februari 22
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema uzinduzi rasmi wa biashara kwa saa 24 utafanyika…
The post Biashara saa 24 kuanza Februari 22 appeared first on HabariLeo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema uzinduzi rasmi wa biashara kwa saa 24 utafanyika Februari 22, 2025 na utaanzia eneo la Ofisini za Mkuu wa Mkoa hadi Kariakoo kuwa na matukio tofauti tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema ufanyaji biashara kwa saa 24 unalenga kuimarisha uchumi wa mkoa, kuongeza mapato ya serikali na kutoa fursa za ajira.
“Ufunguzi huo utaanzia ofisini za Mkuu wa Mkoa hadi Kariakoo ambapo ndipo watafanya ufunguzi rasmi.
Ameeleza kuwa maandalizi ya ufungaji wa kamera za CCTV na taa za barabarani yanaendelea ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unadumishwa.
“Tunahakikisha mkoa wetu wa Dar es Salaam unakuwa na mazingira bora ya kufanya biashara muda wote, na tayari tunashirikiana na viongozi wa halmashauri kuimarisha maeneo yanayofaa kwa biashara za masaa 24,” amesema Chalamila.
“Tutahakikisha tunapanga vizuri maeneo ya chakula pamoja na vinywaji ili kuweka mpangilio mzuri wa biashara hizo kwa kupangilia Usafi.
Aidha ameongeza kuwa mpango huo utaimarisha uchumi na kuwanufaisha wafanyabiashara na wakazi wa jiji hilo.
“Serikali inatarajia kutoa mwongozo mzuri wa ufanyaji biashara na utekelezaji wa mpango huo kabla ya kuanza rasmi Januari 2025,”amesema Chalamila
The post Biashara saa 24 kuanza Februari 22 appeared first on HabariLeo.