Aslay amzungumzia marehemu Pembe

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 13:09:39 EAT   |  Entertainment

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Aslay Isiaka, ameungana na wadau wa burudani katika kuomboleza kifo cha muigizaji mkongwe, mzee Pembe, aliyeaga dunia Jumamosi, Oktoba 20. Aslay amesema kuwa Pembe alijizolea umaarufu sio tu kupitia tasnia ya filamu, bali aliposhirikiana naye katika video ya wimbo wa kwanza wa Aslay, ‘Naenda Kusema kwa Mama’, ambapo aliigiza kama baba …

The post Aslay amzungumzia marehemu Pembe first appeared on HabariLeo.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Aslay Isiaka, ameungana na wadau wa burudani katika kuomboleza kifo cha muigizaji mkongwe, mzee Pembe, aliyeaga dunia Jumamosi, Oktoba 20.

Aslay amesema kuwa Pembe alijizolea umaarufu sio tu kupitia tasnia ya filamu, bali aliposhirikiana naye katika video ya wimbo wa kwanza wa Aslay, ‘Naenda Kusema kwa Mama’, ambapo aliigiza kama baba yake Aslay, anayependa mchepuko kuliko familia.

Aslay ameandika kwenye mtandao wake wa istagramu kwa huzuni akimkumbuka mzee Pembe kama mmoja wa watu muhimu waliochangia mafanikio yake katika safari ya muziki.

“Moja kati ya watu waliotengeneza barabara ya maisha yangu ya mziki ni huyu Mzee Pembe. Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake,” aliandika Aslay huku akionyesha hisia zake za majonzi.

Aliendelea kwa kumtakia mzee Pembe pumziko la amani: “Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee wetu Pembe mahali pema peponi. Pole ziwaendee familia yake na wapenda burudani wote.”

Mzee Pembe alikuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya maigizo, hususan vichekesho, na kifo chake kimeacha pengo kwa familia yake, wasanii, na wapenzi wa sanaa kwa ujumla.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Aslay (@aslayisihaka)

The post Aslay amzungumzia marehemu Pembe first appeared on HabariLeo.