Askofu Bendera ahimiza amani uchaguzi mkuu 2025

ASKOFU wa Kanisa la Ufunuo Tanzania ambaye anasimamia Mkoa wa Shinyanga Samawi Bendera amewataka watanzania kuishi kwa amani…
The post Askofu Bendera ahimiza amani uchaguzi mkuu 2025 appeared first on HabariLeo.
ASKOFU wa Kanisa la Ufunuo Tanzania ambaye anasimamia Mkoa wa Shinyanga Samawi Bendera amewataka watanzania kuishi kwa amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
Askofu Bendera amesema hayo kwenye ibada maalum ya kusimikwa wachungaji 14 waliopata mafunzo ya kiuchungaji katika chuo cha kanisa hilo campas ya Kahama kwa kipindi cha mwaka mmoja huku akiwasisitiza kutojihusisha na masuala ya kisiasa nakufuata sheria, kanuni na taratibu za kanisa.
Bendera amesema wachungaji sasa wamesimikwa rasmi kujitoa kusimamia neno la Mungu wanatakiwa kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura nakumchagua kiongozi anayefaa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuendelea kutoa elimu ya kutokwenda kwa waganga wa kienyeji ambao wanaleta uhasama,chuki na watu kukosa amani.
“Baada ya kula kiapo maalum cha kiuchungaji nakupatiwa vyeti mmekuwa wachungaji sasa mnayo nafasi ya kuwa watumishi wenye unyenyekevu mbele za watu nakuendelea kuhubiri neno la mungu kwani aliyewachagua mpaka hapo walipofikia ni yeye” amesema Bendera.
Askofu wa jimbo la Mwanza ambaye ni katibu wa kanda ya Ziwa Uvumi Paul wakati akitoa nasaha kwa wachungaji hao amesema waende wakaishi maishi yenye unyenyekevu na utii wasiende kuutumia utumishi wao kwa kutanguliza pesa wahakikishe wanakwenda pia kuitetea amani ya nchi hii.
Katika ibada hiyo mgeni rasmi Askofu Lyidia John akimwakilisha Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Paul Bendera amesema sasa wamekubaliwa kuingia kwenye shamba la mungu kinachotakiwa ni kufuata misingi ya utumishi nakuwa wadogo kwa wengine pia kujitoa sadaka.
“Wanatakiwa kujiuliza kwa nini mungu amewaita kwenye mikono yake na ndivyo wakalitukuze neno lake kwa kuwafundisha watu wasipotoke na matendo maovu nakudumisha amani ya nchi, “amesema John.
Mchungaji Charles Bundala aliyesimikwa kwenye ibada hiyo amesema wito,uvumilivu na utii ndiyo umewafanya kumpokea mungu kwani wapo waliokwama njiani lakini aliahidi kushirikiana na watu wote kwenye maeneo aliyopo ili kuendeleza umoja na mshikamano.
Mchungaji Veneranda Maganga alisema ana mshukuru mungu na uongozi wa kanisa kwa kuwasimamia vizuri watakwenda kuyaishi mema ya mungu nakufuata sheria,kanuni na taratibu za kanisa pia kuendelea kusisitiza amani zaidi.
The post Askofu Bendera ahimiza amani uchaguzi mkuu 2025 appeared first on HabariLeo.