Anzisheni kozi zitakazochangia maendeleo ya nchi :Rais Mwinyi

Milard Ayo
Published: Oct 19, 2024 12:35:06 EAT   |  Educational

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezishauri taasisi za elimu ya juu zilizo nchini kuanzisha kozi muhimu zenye uhitaji na uhaba wa wataalamu, ambazo zitachangia ya nchi. Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia sekta ya afya kuwa na wataalamu wa kutosha katika kada mbalimbali, watakaotoa […]

The post Anzisheni kozi zitakazochangia maendeleo ya nchi :Rais Mwinyi first appeared on Millard Ayo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezishauri taasisi za elimu ya juu zilizo nchini kuanzisha kozi muhimu zenye uhitaji na uhaba wa wataalamu, ambazo zitachangia ya nchi.

Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia sekta ya afya kuwa na wataalamu wa kutosha katika kada mbalimbali, watakaotoa huduma kwa kuzingatia utaalamu na weledi, hivyo kuimarisha sekta ya afya

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo kwenye mahafali ya 12 ya Zanzibar School of Health leo, tarehe 19 Oktoba 2024, katika viwanja vya Mao Tse Tung, Mkoa wa Mjini Magharibi.


Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa wahitimu wa kada tofauti wazingatie nidhamu na maadili ya kazi katika utoaji wa huduma wanapoingia kwenye majukumu yao, na kuwa msaada muhimu kwa jamii.

Aidha, amewasisitiza vijana kusoma kozi zenye umuhimu na uhitaji, hususan zinazoanzishwa na Zanzibar School of Health, huku akiipongeza juhudi zinazochukuliwa na chuo hicho kuanzisha kozi mpya.

Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi amefafanua kuwa juhudi hizo zinaendana na malengo ya Serikali ya kuhakikisha chuo hicho kinakuwa chemchem ya kuzalisha wataalamu katika sekta ya afya.

Vilevile, ametoa wito kwa wahitimu wa chuo hicho kujiendeleza zaidi kielimu pale fursa zinapojitokeza.

The post Anzisheni kozi zitakazochangia maendeleo ya nchi :Rais Mwinyi first appeared on Millard Ayo.