Amaan  yachangamka mapema, mashabiki Simba waonyesha vidole vitatu

Mwanaspoti
Published: May 25, 2025 11:18:31 EAT   |  Sports

LEO ni siku ya kihistoria katika ardhi ya visiwa vya Zanzibar. Uwanja wa New Amaan, uliopo Unguja umebeba matumaini kwa mashabiki wa Simba, ambao wamefurika kwa maelfu wakiwa na lengo moja tu kushuhudia timu yao ikipindua meza dhidi ya RS Berkane ya Morocco na kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika.