Alienda miguu peku utotoni, sasa anavalisha wengi viatu
KATIKA dunia ya sasa, uwezo wa kuvumbua na kutumia tena bidhaa zilizokwisha kutumika (kuchakata upya) kutengeneza bidhaa nyingine, ni njia moja ya kukabiliana na uchafuzi unaosababishwa na uchafu wa plastiki.
Kwa Bw Hamisi Juma Gonda mmiliki wa biashara ya AlMercy, ubunifu wa kutumia vipande vya magurudumu ya gari kutengeneza viatu, unamsakia tonge katika nyakati hizi ambazo ajira imeadimika.
Kwa Bw Gonda, mapenzi haya yalianza miaka ya awali akiwa katika shule ya msingi ya Shamu, Kaunti ya Kwale alipotaka kukwepa aibu ya kuenda shuleni bila viatu.
Anaeleza Taifa Leo kwamba miaka yake ya kwenda shule akiwa kijana mdogo hakuwahi kuvalia viatu hadi alipofika darasa la nane.
Bw Gonda anaeleza kwamba familia yake haikumudu bei ya viatu hivyo basi alilazimika kutembea nyayo zikikanyaga chini licha ya jua kali.
“Maisha yetu kama familia yalikuwa magumu sana na wazazi wangu hawakujiweza. Ilibidi niingie msalani bila viatu, jambo ambalo liliniweka katika hatari ya kupata magonjwa. Kiatu cha jirani yangu kilichotengenezwa na kipande cha gurudumu kilinipendeza ndiposa nikataka kukitengeneza,” anasema Bw Gonda.
Kutengeneza kiatu cha kwanza
Kwa mujibu wake, hatua ya kutengeneza kiatu cha kwanza kulimchochea kutengeneza viatu ili yeyote asiwahi kukosa viatu.
“Nilitafuta jinsi nitakavyotatua shida iliyonikumba ili wanafunzi wengine wasiipitie pia na kusaidika kuzingatia kwamba mitaa yetu watu ni wa mapato ya chini,” alisema.
Gonda, 29, anahoji kuwa mapenzi yake kwa sanaa ya kutengeneza viatu yaliongezeka baada ya wenzake kupenda kiatu alichotengeneza kujisitiri na kuomba awauzie.
“Nikiwa katika shule ya msingi eneo la Ukunda, nilitengeneza jozi moja ya viatu wakati wa wikendi, nilipoenda navyo shule vikanunuliwa na nikarejea nyumbani miguu chuma na kutengeneza jozi nyingine moja,” anasema Bw Gonda.
Bw Gonda anasema jambo hilo lilimfurahisha sana kwani wenzake waliweza kupata viatu vya kwenda shuleni.
Bw Gonda anaeleza ili kuanzisha biashara yake rasmi baada ya kumaliza kidato cha nne mnamo 2014, alipewa mtaji wa Sh500 na mama yake mzazi ili aanzishe biashara hiyo, jambo ambalo hawezi kulisahau asilani.
Alipoanzisha biashara yake ya kutengeneza viatu miaka 10 iliyopita, Bw Gonda anasema kuwa ili ahifadhi mazingira, alitumia malighafi ya magurudumu yaliyotumika ili kujikimu kimaisha.
“Nilitumia magurudumu yaliyotumika kwa muda, lakini baadaye wateja wengine walilalamika kuhusu uzito wa malighafi hayo, hali iliyonilazimu kutafuta ngozi halisi ambayo niliweka upande wa juu wa kiatu na kuweka gurudumu mahali pa kukanyagia,” anaeleza Bw Gonda.
Mafunzo ya juakali
[caption id="attachment_163212" align="alignnone" width="300"] Baadhi ya bidhaa za viatu katika duka la Hamisi Gonda eneo la Likoni, Kaunti ya Mombasa. Picha|Mkamburi Mwawasi[/caption]Bw Gonda alipata mafunzo ya uanagenzi kwa fundi wa juakali ambaye alimfunza na kumpa elimu zaidi ya kutengeneza viatu mbalimbali.
“Baada ya hapo nilijiunga na chuo cha NITA ili kujiendeleza kielimu na sasa niko daraja ya tatu katika masomo yangu. Ningependa kuwaeleza vijana kwamba kazi za kujiajiri zipo na wasitegemee elimu tuliyotoka nayo shuleni tu,” alisema.
Akiwa dukani kwake maeneno ya Likoni, Bw Gonda alisema mteja anaweza kutengezewa kiatu kwa mtindo anaotaka. Viatu vyake ambavyo ni vya watoto, wanawake na hata wanaume, huuzwa kwa kati ya Sh400 hadi Sh1,500.
Mwaka huu, lengo la Bw Gonda lilikuwa kuleta bidhaa mpya ambayo ni ya viatu vya shule.
Anaeleza kwamba viatu hivyo vitakuwa vinauzwa kwa bei nafuu ili kumaliza idadi ya wanafunzi wanaotembea miguu pekupeku wakienda shuleni.
Bw Gonda anawarai vijana wafikirie jinsi ya kujiajiri na kuepuka uhalifu, akiongeza kwamba vijana wanaofuzu kila mwaka ni wengi, ila nafasi za ajira ni nadra.
“Kuna vitu vingi sana vinavyoweza kutengenezwa kutokana na malighafi ya magurudumu. Kwa hivyo vijana wanafaa kutambua kwamba kuna nafasi za kujiajiri na kujikimu kimaisha bila kuwapora watu wengine,” akasema.
Anaeleza kwamba mbali na magurudumu yaliyotumika kutengeneza viatu, yanaweza pia kuunda bidhaa kama meza, viti, shamba dogo la nyumbani upande wa jikoni, iwapo kijana ni mbunifu.
Atafungua maduka mengine
Bw Gonda ana matumaini kwamba miaka ijayo atafungua maduka mengine maeneo ya Kwale na Bamburi.
Anaeleza kuwa wateja wameshaanza kuagiza viatu vya watoto wa shule kupitia kwa mitandao yake ya kijamii, akiongeza kwamba mtandao ndio moja wapo ya njia inayofanya biashara yake kunawiri.
Katika duka lake, Bw Gonda ameandika wafanyikazi wanne, wakiwemo wanawake wawili na wanaume wawili wanaomsaidia katika shughuli za kila siku. Anasema kuwa katika miezi ambayo biashara haijanoga sana, yeye hujiingizia takriban Sh40,000.
Fundi huyu anataja kuadimika kwa malighafi ya magurudumu kama changamoto kuu katika biashara yake, jambo ambalo wakati mwingine humrejesha nyuma.
Kijana huyo anashukuru shirika la Somo Africa kwa mafunzo aliyopata manmo 2019 na 2020 yaliyomsaidia kuendeleza biashara yake.
“Namna nilivyokuwa nikifanya biashara hapo awali ni tofauti na sasa baada ya kupitia masomo ya kibiashara ya Somo Africa. Sasa hivi nimefungua mitandao ya kijamii ya kuendeshea biashara. Kwa mafunzo hayo, sasa ninaweza hata kuweka rekodi za biashara yangu na kupitia stakabadhi za biashara kuwa na ufahamu wa nilipofanya vizuri na wapi kwa kuongeza juhudi,” asema.
Mfanyakazi mmoja wa Bw Gonda Bi Jamila Juma ambaye ana asili na usuli wake nchini Tanzania, anaeleza kuwa kazi hiyo imempa mtazamo tofauti wa kibiashara.
Sharubati na mabuyu
“Nilipata kazi hii kupitia kaka yangu baada ya kukaa nyumbani kwa miaka kadhaa bila kupata kazi. Mbali na kuuza katika duka hili, nimeweka sharubati na mabuyu ili niongeze mapato,” anasema Bi Juma.
Bi Jamila alitaja jinsi sarafu za Kenya zilivyomchanganya alipowasili katika kazi hiyo miezi ya kwanza, lakini kupitia msaada aliopata kutoka kwa Bw Gonda ameweza kuzielewa.
Mwanzilishi wa shirika la Somo Africa Bi Amelia Hopkins anasema Bw Gonda ni mmojawapo wa vijana waliopokea masomo ya kuanzisha na kukuza biashara zao na anafanya vyema sana.
“Ni mpango unaonuia kufikia vijana wa mashinani na kuwafunza jinsi ya kuendesha biashara zao, kuweka rekodi, kufungua mitandao na kukuza mauzo. Yaani kupanua biashara na kujijenga hata zaidi,” anasema Bi Hopkins.
Anaongeza kwamba biashara za kibinafsi ni mojawapo ya njia ya kukusanya mali na kutengeneza nafasi za ajira na kubadilisha maisha ya jamii.