Ali Kiba atunukiwa tuzo na wanawake Zanzibar

Habari Leo
Published: Oct 21, 2024 14:19:51 EAT   |  Entertainment

MWIMBAJI wa Bongo Fleva nchini Ali Kiba ‘King Kiba’ ametunukiwa tuzo Bingwa wa Maendeleo ya Mtoto wa Kike kupitia Kongamano la Kigoda cha Wasichana kilichofanyika Visiwani Zanzibar. Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Shiraz Foundation imemkabidhi tuzo hiyo Ali Kiba alipohudhuria na kushiriki Kongamano hilo viwanja vya Nyamanzi Zanzibar. Katika Kongamano hilo ambalo mgeni rasmi, Waziri …

The post Ali Kiba atunukiwa tuzo na wanawake Zanzibar first appeared on HabariLeo.

MWIMBAJI wa Bongo Fleva nchini Ali Kiba ‘King Kiba’ ametunukiwa tuzo Bingwa wa Maendeleo ya Mtoto wa Kike kupitia Kongamano la Kigoda cha Wasichana kilichofanyika Visiwani Zanzibar.

Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Shiraz Foundation imemkabidhi tuzo hiyo Ali Kiba alipohudhuria na kushiriki Kongamano hilo viwanja vya Nyamanzi Zanzibar.

Katika Kongamano hilo ambalo mgeni rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (SMZ) Riziki Pembe, Mgeni Maalum na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zena Said na Mgeni Maalum na Mlezi wa Jukwaa hilo Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Juma.

Alikiba alipongeza jukwaa hilo la Kigoda cha Wasichana na kuahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika mambo mengine ya Kijamii na kuendelea kumuwezesha mtoto wa kike.

“Nitaendelea kushirikiana nanyi katika kusaidia na kumuenzi mtoto wa kike wakati wote kwa kuwa ndio kiongozi mama wa familia ya baada mwenye majukumu mengi zaidi,” amesema

The post Ali Kiba atunukiwa tuzo na wanawake Zanzibar first appeared on HabariLeo.