Ajira mpya 74,000 zaja

Habari Leo
Published: Apr 24, 2025 08:18:14 EAT   |  Jobs and Career

SERIKALI inatarajia kutoa vibali vya ajira mpya 41,500 katika mwaka wa fedha 2025/2026. Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan…

The post Ajira mpya 74,000 zaja appeared first on HabariLeo.

SERIKALI inatarajia kutoa vibali vya ajira mpya 41,500 katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha, Rais Samia Suluhu Hassan juzi alitoa kibali cha kua jiriwa watumishi wapya 33,212 katika mwaka huu wa fedha unaoishia Julai.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utu mishi wa Umma na Utawala Bora), George Simbachawene alibainisha hayo jana wakati akiwasilisha bungeni Makaribio ya Mapato na Matumizi ya ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Ofisi hiyo imeomba kuid hinishiwa Sh 1,354,350,324,000. Kati ya kiasi hicho, Sh 1,171,035,237,000 ni matumizi ya kawaida na Sh 183,315,087,000 ni za miradi ya maendeleo.

“Katika mwaka 2025/2026 Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imepanga kushughulikia vibali 41,500 vya ajira ili kujaza nafasi zilizoidhinishwa katika ikama,” alisema Simbachawene.

Sambamba na hilo, alisema katika mwaka ujao wa fedha ofisi hiyo pia itafanya uhakiki maalumu wa watumishi katika taasisi za umma za Mkoa wa Dodoma. Alisema pia, itafanya uhakiki na kuidhinisha madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi kwa taasisi 425 pamoja na kusafisha taarifa za kiutumishi na mishahara kwa watumishi waliopo katika taasisi 433 zinazotumia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Misha hara (e-Watumishi).

Simbachawene alisema mambo mengine yatakayofany wa ni kuhakiki na kuidhinisha mabadiliko ya taarifa zinazohu su utumishi na mishahara katika Mfumo wa e-Watumishi kwa taasisi 524, kuwezesha taasisi 35 ambazo kwa sasa hazitumii mfumo huo kuanza kuutumia katika kusimamia masuala ya kiutumishi na mishahara.

“Tutafanya uchambuzi wa miundo ya wizara na taasisi za umma 30 baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025,” alisema Simbachawene.

Pia, kutajengwa mfumo utakaounganisha mifumo ya Tehama ya sekta ya utumishi na utawala bora utakaorahisisha ubadilishanaji wa taarifa baina ya mifumo iliyopo ndani na nje ya sekta ya utumishi na utawala bora.

Akisoma maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Makamu Mwenyekiti wake, Florent Kyo mbo alitaka serikali itengeneze mfumo wa malipo ambao utakuwa ni mwongozo kwa ofisi za umma na serikali kwa lengo la kuwasaidia vijana wanaoji tolea katika nafasi mbalimbali.

Vibali ajira 33, 212

Kuhusu kibali cha kuajiri watu mishi wapya 33,212 kilichotole wa juzi na Rais Samia, akihiti misha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya ofisi yake, Simbachawene alisema kati ya hao wapya wamo walimu 10,000 na wataajiriwa bila kufanyiwa usaili na serikali itawachukua kwenye kanzidata yake. Alisema si rahisi serikali kua jiri wahitimu wake wote, hakuna serikali imeweza kufanya hivyo duniani bali ameitaka sekta binafsi iendelee kuimarishwa ili iendelee kuajiri wahitimu zaidi.

“Tusihesabie kuwa na wahitimu wengi kama mkosi na kujutia, bali tuendelee kutafuta namna ya kupata ajira,” alisema.

Ajira za kujitolea zaja

Aidha, alisema kuanzia Julai mwaka huu mwongozo wa ajira za kujitolea utaanza rasmi kufanya kazi na watakaojitolea watapatiwa stahiki zao ikiwemo fedha za kujikimu.

“Katika utumishi wa umma hakuna msamiati wa ajira za muda na ndio tumekuja na msamiati wa ajira za kujitolea, sasa tutaweka mfumo wa kupata stahiki za kujikimu. Umewekewa muongozo ili wanaojitolea watendewe haki,” alisema.

The post Ajira mpya 74,000 zaja appeared first on HabariLeo.